• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 2:33 PM
Walioshutumu Nyeri kwa kuajiri washika panya…New York pia yaajiri mshika panya

Walioshutumu Nyeri kwa kuajiri washika panya…New York pia yaajiri mshika panya

MERCY KOSKEI NA MASHIRIKA 

JIMBO la New York, Amerika limeaajiri ‘mshika panya’ wa kwanza kusaidia kupambana na ongezeko la panya katika jiji hilo lenye idadi ya juu ya watu.

Meya Eric Adams ametengaza kumteua Kathleen Corradi, mfanyakazi wa idara ya elimu, kuwa mtega panya.

Hatua ya kuajiri mshika panya, ni kisa cha kwanza kabisa kuripotiwa New York.

Bw Adams, ambaye mara nyingi ameonyesha chuki kubwa kwa panya, alichapisha nafasi ya kazi hiyo mwaka jana, akitafuta mtu ‘mwenye kiu cha umwagaji damu’.

Meya huyo alitoa ahadi ya msharahara wa kuvutia, Dola kati ya 120,000 – 170,000.

Malipo hayo ni sawa na Sh16, 095, 747 – 22, 802, 308 thamani ya Kenya.

Miezi kadhaa baadaye, nafasi iyo imepata mtu.

Corradi, mwalimu wa zamani, si mgeni katika vita dhidi ya panya. Hapo awali alisimamia juhudi za kupunguza panya katika shule za umma New York.

Akihutubia wanahabari Corradi ambaye jina lake rasmi ni ‘mkurugenzi wa kudhibiti panya katika jiji lote’, alihakikishia wakazi kuwa atafanya jukumu alilopewa na kuhakikisha kuwa panya wamepungua na watu kuongezeka.

Kulingana na data ya jiji la New York, ongezeko la panya limeshudiwa katika miaka ya hivi karibuni na kulazimu kutafuta mbinu ya kukabiliana na wanyama hao waharibifu.

Maafisa wengine wanasema kuongezeka kwa mikahawa ya njiani kumechangia shida hiyo.

“Idadi ya panya kwenye jiji hili haijulikani, ila utafiti wa 2014 uliweka takwimu kuwa karibu milioni 2 au 1 kwa kila wakazi wanne,” alisema Adams

Adams pia ametekeleza hatua zingine zinazolenga kile alichokiita ‘New York  Adui Namba Moja’.

Miezi kadha iliyopita, utawala wa Adams umepunguza muda ambao mifuko ya takataka inaweza kukaa kando ya barabara ikisubiri kuchukuliwa na kuzindua mpango wa kutengeneza mboji unaolenga kupunguza upotevu wa chakula.

Panya wa kahawia, ambaye huenda alifika New York wakati wa Vita vya Mapinduzi, amethibitishwa kuwa adui mjanja, anayestawi licha ya majaribio mengi ya kumuangamiza kutoka kwa vichuguu vya jiji la ardhi na vichochoro.

  • Tags

You can share this post!

Wakazi wa Shakahola wataka serikali iwajengee kituo cha...

Idadi jumla ya walioangamia Shakahola sasa ni 73

T L