• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 7:53 AM
Wakazi waambukizwa ugonjwa hatari kwa kutumia maji pamoja na wanyama

Wakazi waambukizwa ugonjwa hatari kwa kutumia maji pamoja na wanyama

NA SAMMY LUTTA

MARADHI yasiyo ya kawaida yenye dalili za vipele, magoti dhaifu, homa na kutapika, yamewakumba wakazi wanaoishi katika kijiji cha Kibish kinachokabiliwa na uhaba wa maji kwenye mpaka wa Kenya na Ethiopia.

Hii ni baada ya wafugaji zaidi ya 3, 000 kuhamia kwenye chemchemi ya Natapar ambayo kando na kuwa tegemeo la maji ya matumizi ya kinyumbani na mifugo inatumiwa pia na mbwa na wanyamapori.

Mchungaji aliyehamia eneo hilo Agosti 2023, Albert Loperito, anasema licha ya maji hayo kuwa na rangi ya kijani kibichi na kujaa matope kutokana na udongo, mtu yeyote au mnyama anayetaka kukata kiu ni sharti atumbukize miguu yote majini.

“Hakuna chemichemi nyingine yoyote ya maji na sawa na mbwa, mifugo na wanyamapori, mimi pia hukanyaga maji ili kukata kiu changu. Nina vipele, kuendesha, kutapika na siwezi nikatembea kwa muda mrefu kutafuta malisho,” alisema Bw Loperito.

 

  • Tags

You can share this post!

Kiptum sasa ndiye mfalme mpya wa marathon duniani

Akothee adai kuwa mjamzito baada ya kuachana na mumewe...

T L