• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 6:55 PM
Wanavoliboli wa Kenya ya ufukweni hawana corona, watawania tiketi ya Olimpiki

Wanavoliboli wa Kenya ya ufukweni hawana corona, watawania tiketi ya Olimpiki

Na AGNES MAKHANDIA akiwa Agadir, Morocco

TIMU za Kenya za voliboli ya ufukweni zinaweza sasa kupumua baada ya matokeo ya msafara wake mzima ya virusi vya corona kuonyesha hakuna aliye navyo.

Wakenya walipimwa katika uwanja wa ndege wa Rabat mara tu walipowasili mnamo Jumapili asubuhi baada ya kusafiri Ijumaa kupitia nchini Ufaransa.Shirikisho la Voliboli Afrika (CAVB) limethibitisha kuwa mataifa 15 ya wanaume na 10 ya wanawake yatashiriki mashindano ya Afrika ya voliboli ya ufukweni ya kufuzu kushiriki Olimpiki.

Yataandaliwa mjini Agadir, Morocco mnamo Juni 22-28.Mashindano ya wanaume yalitarajiwa kuwa na mataifa 20, lakini Mauritius, Sudan Kusini, Cape Verde na Sierra Leon hazikujitokeza nao Tanzania walijiondoa kutokana na uhaba wa fedha.

Watakaopigania tiketi ya wanaume ni Kenya pamoja na Morocco, Msumbiji, Ghana, Rwanda, Nigeria, Afrika Kusini, Tunisia, Sudan, Misri, Togo, DR Congo, Congo Brazzaville, Mali na mabingwa wa Afrika, Gambia.Mashindano ya kinadada yatahusisha Kenya, Nigeria, Misri, Msumbiji, Rwanda, Gambia, Cape Verde, DR Congo, Sudan na Morocco baada ya Afrika Kusini, Mali, Mauritius, Tunisia, Ivory Coast, Niger na Zambia kukosa kujitokeza.

Mkutano wa washiriki unatarajiwa kuandaliwa Juni 21 usiku.Kocha wa timu ya wanawake ya Kenya, Sammy Mulinge ametaka vipusa wake wajitahidi kupata matokeo mazuri. Kenya inawakilishwa katika kitengo hicho na Gaudencia Makokha atakayeshirikiana na Brackcides Agala, na Phoscah Kasisi atakayefanya kazi na Yvonne Wavinya.

“Tulifanya kila kitu tulihitaji kufanya mazoezini nchini Kenya na hakuna mapya ya kufanya mazoezini hapa isipokuwa kufanya majaribio katika viwanja vitakavyotumiwa. Matumaini yangu ni kuwa tutapata droo nzuri,” alisema Mulinge.

Mwenzake kutoka timu ya wanaume, Patrick Owino alisalia mwingi wa matumaini akisema kuwa vijana wake wanafahamu umuhimu wa kuandikisha matokeo mazuri.”Tumetafuta fursa hii kwa muda mrefu. Sasa tumeipata na hatuna budi, bali kufanya vyema,” alisema Owino.

Kenya itawakilishwa na Ibrahim Oduori atakayeshirikiana na James Mwaniki, na Brian Melly na Enock Mogeni.

  • Tags

You can share this post!

Chipukizi wa AFC Leopards Youth wazidi kutamba Ligini

MICHEZO: Kiota ambacho kinaelekea kufikia malengo ya...