• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 12:09 PM
Waomba bangi ikubaliwe kufanyia ibada

Waomba bangi ikubaliwe kufanyia ibada

Na RICHARD MUNGUTI

WAUMINI wa Imani ya Rastafari (RSK) Jumatatu waliwasilisha kesi wakiitaka Mahakama Kuu ihalalishe matumizi ya bangi wakisema inawasaidia wanapoabudu.

Kupitia wakili Shadrack Wamboi, walidai kuwa bangi ni dawa na ina nguvu za kiroho zinazowawezesha kuwasiliana na Mungu.

Wanasema sheria ya kupambana na ulanguzi wa mihadarati na vileo iliyopitishwa mwaka wa 1994 inawabagua.

Pia waumini hao wanadai kwamba haki zao za kimsingi na kikatiba zinakandamizwa, ilhali Katiba ya 2010 imetoa uhuru wa kuabudu.

RSK pamoja na kiongozi wao, Nabii Mwendwa Wambua (Ras Prophet) wanaomba mahakama ipeleke kesi yao kwa kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu ateue jopo la majaji watatu au zaidi wasikilize kesi yao.

Chama hicho cha marasta kiliandikishwa katika ofisi ya msajili wa vyama mnamo 2017.

Waumini wa Urastafari wako na hekalu mahala kwingi nchini ikiwa ni pamoja na mjini Wote, Kaunti ya Makueni na Nairobi.

Kesi hiyo itatengewa siku ya kusikilizwa na Jaji katika idara ya kuamua kesi za haki za binadamu.

You can share this post!

TAHARIRI: Mjadala wa bangi ufanywe kimakinifu

Gavana wa Wajir atimuliwa afisini