• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 7:53 PM
Wasichana zaidi ya 5,000 waepuka kukeketwa, ndoa

Wasichana zaidi ya 5,000 waepuka kukeketwa, ndoa

Na OSCAR KAKAI

ZAIDI ya wasichana 5,000 katika Kaunti ya Pokot Magharibi wameokolewa kutoka kwa ukeketaji na ndoa za mapema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Haya yalifichuliwa na mratibu wa shirika la Pokot Girl Child Network, Bi Teres Lokichu, kwenye mkutano wa kuhamasisha jamii juu ya athari za ukeketaji uliofanyika Chepareria.

Bi Lokichu alisema kuwa zaidi ya asilimia kumi ya wasichana wenye umri mdogo wamepashwa tohara kisiri.Alisema kuwa mashirika ya kijamii yameokoa zaidi ya wasichana 5,000 ambao walikuwa wamelazimishwa kukeketwa.

You can share this post!

TAHARIRI: Sharti amani idumishwe mikutano ya kisiasa leo

Wawekezaji walilia Balala aokoe utalii

T L