• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 4:26 PM
Waziri Mkuu wa Algeria ajiuzulu

Waziri Mkuu wa Algeria ajiuzulu

Na XINHUA

Tafsiri: CHARLES WASONGA

ALGIERS, Algeria,

WAZIRI Mkuu wa Algeria Abdelazizi Djerad na wanachama wa baraza lake la mawaziri waliwasilisha barua zao za kujiuzulu kwa Rais Abdelmadjid Tebboune Alhamisi, runinga ya ENTV iliripoti.

Kulingana na kipengele cha 113 cha Katiba, Mawaziri hujiuzulu baada ya matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa ubunge kuthibitishwa.Kwa hivyo, kujiuzulu kwa Djerad na mawaziri wake kunajiri baada ya  kutangazwa kwa matokeo rasmi ya uchuguzi wa ubunge uliofanyika Juni 12.

Matokeo hayo yalitangazwa na mahakama ya kikatiba Jumatano jioni.Katiba hiyo pia inasema katika kipengele cha 103 kwamba serikali inaongozwa na Waziri Mkuu ikiwa chama cha Rais kimeshinda viti vingi bunge. Serikali itaongozwa na kiongozi wa serikali ikiwa chama cha upinzani kimepata idadi ya juu ya viti bungeni.

Rais Tebboune  alimwomba Djerad na mawaziri wake kusalia afisini hadi serikali mpya itakapoundwa lakini akakaidi ombi hilo.Mnamo Jumatano jioni, kulitangazwa kuwa chama cha National Liberation Front (FLN) kilipata viti 98 kati ya jumla ya viti 407 katika bunge la chini.

Wagombeaji huru nao walipata viti 84 huku chama kinachoegemea dini ya kiislamu cha Movement of Society for Peace (MSP) kilipata viti 65. Chama tawala cha zamani, National Democratic Rally (RND) kilipata viti 58.Chama cha El Moustakbal Front kilipata viti 48 huku kile cha El Binaa Movement kikapata viti 39.

Viti 15 vilivyosalia vilitwaliwa na vyama vidogo.Matokeo ya uchaguzi huo ni ya kipekee kwa sababu kwa mara ya kwanza wagombeaji huru wamekuwa wa pili katika idadi ya wabunge katika Bunge la Algeria tangu nchi hiyo ikumbatie siasa za vyama vingi mnamo 1989.

  • Tags

You can share this post!

Eti ni nadhifu, tupelekane wapi?’

Safari Rally balaa!