• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Waziri wa Afya asihi wakazi wakuze miti kwa matumizi ya dawa

Waziri wa Afya asihi wakazi wakuze miti kwa matumizi ya dawa

NA TITUS OMINDE

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amefichua kuwa Kaunti ya Elgeyo/Marakwet itakuwa kipaumbele katika upanzi wa miti ambayo itatumika kwa thamani ya dawa ili kutumika kama malighafi ya kutengeneza dawa za mitishamba.

Akizungumza katika kituo cha msitu cha Kipkabus Kaunti ya Elgeyo/Marakwet, wakati wa Sikukuu ya Kitaifa ya Upandaji Miti, Bi Nakhumicha alieleza haja ya kupanua upanzi wa miti ya kiasili ili itumike kwa thamani ya dawa.

Bi Nakhumicha alisema kuwa asilimia kubwa ya zaidi ya miti 50 milioni ambayo serikali inanuia kuipanda katika kaunti hiyo kupitia ushirikiano na Kenya Medical Research (KEMR) itakuwa miti ya kiasili itakayotumika kama malighafi ya dawa za mitishamba na thamani nyingine za matibabu.

“Tunakusudia kupanda zaidi ya miti ya kiasili milioni 50 katika nchi hii kwa miaka 10 ijayo. Miti hiyo mingi itatumika kwa madhumuni ya dawa na utafiti na KEMRI,” alisema Bi Nakhumicha.

Wakati huo huo, Bi Nakhumicha aliagiza watumishi wote wa Afya ya Jamii CHP katika Kaunti ya Elgeyo/Marakwet kuhakikisha miche zaidi ya milioni 50 ambayo serikali inanuia kuipanda katika kaunti hiyo katika muda wa miaka 10 ijayo, inanawiri hadi ikomae.

Vile vile, aliondoa hofu ya kutokea uhababa wa miche kwa kutilia mkazo kwamba jamii inahusishwa kwa upanzi wa miche ambazo zitatumika kama mbegu ya miti kote nchini.

  • Tags

You can share this post!

Kenya Power yamulikwa kwa madai ya kuitisha hongo ya Sh200,...

Wanajeshi 2 wa Uganda wahukumiwa kwa kutoroka Al-Shabaab...

T L