• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 9:11 AM
Wito kwa walemavu wajiunge na miradi ya maendeleo

Wito kwa walemavu wajiunge na miradi ya maendeleo

Na SAMMY KIMATU

NAIROBI

WALEMAVU wameshauriwa kuungana kuanzisha vikundi vya miradi ya kutengeneza mapato ili wajiinue kiuchumi sawia na kuimarisha maisha yao.

Aidha, waliulizwa kuanzisha vikundi vya wanachama kuanzia watu kumi kwenda juu ili waombe mikopo ya serikali kwa manufaa ya kujisaidia.

Hayo yalinenwa jana na mwakilishi wa wadi ya Nairobi South , ilioko kwenye kaunti ndogo ya Starehe, Bi Waithera Chege.

Bi Chege alisema hayo katika mkutano na walemavu zaidi ya 50 kutoka tarafa ya South B.

Kwenye hafla hiyo, Bi Waithera aliwapatia chakula cha msaada kutoka kwa ofisi ya kaimu gavana wa Nairobi B, Anne Kananu.

’’Serikali ina pesa nyingi za kuwafaidi wananchi. Jiungeni na vikundi vilivyo na nia ya kutengeneza pesa. Kisha chukueni mikopo kutoka kwa serikali ya kitaifa ili mjisukume kimaendeleo, ‘’ Bi Waithera akasema.

Mkutano huo ulifanyika nje ya afisi yake katika mtaa wa Plainsview ulioko South B.

Kuhusu habari za mikopo, aliwafafanulia kuwa kuna Hazina ya Uwezo, Hazina ya Vijana, Hazina ya Akinamama na mikopo ya serikali kwa watu binafsi pia.

‘’Serikali kuu ya Kenya ina hazina mbalimbali kwa minajili ya kuinua watu wake. Kuna haziya ya wanawake, hazina ya vijana Hazina ya uwezo na pia kuna mikopo kwa wafanyabiashara binafsi waliostawi kazini,‘’ diwani huyo alisema.

Mwanasiasa huyo aliwauliza viongozi wengine, makanisa, misikiti, mkapuni na wahisani wengine kuwasaidia wasiobahatika katika jamii wakati huu janga la Corona imevuruga uchumumi.

Aliongeza kwamba inahuzunusha kuwaona wakenya wakilala njaa baada ya wengi wao kufutwa kazi kutoka kwa makampuni kwenye Eneo la Viwandani na kwingineko.

“Kusema ukweli watu wengi wanahangaika kwa ukosefu wa chakula baada ya janga la Corona huku wengi wakifutwa kazini walikiopata mkate wao wa kila siku,’’ Bi Waithera akasema.

Kuhusu uhalifu, mwanasiasa huyo alikariri kwamba uhalifu umepungua katika wodi yake baada ya vijana kujiunga na kazi mtaani.

Kando na walio kwenye kazi mtaani, kuna vijana zaidi 350 kwenye mradi wa mwanasiasa huyo ambao hung’arisha mitaa na barabara katika maeneo ya South B.

Isitoshe, vijana hao walipata kazi hiyo miaka minane kabla ya Bi Waithera kuchaguliwa kam mbunge wa kaunti.

Vilevile, mbunge huyo na mradi wa kuwabadilisha waliokuwa wakiijiingiza kufanya uhalifu na kuwapatia mbinu badala ya kujitafutia bila kutenda uhalifu.

Fauka ya hayo, aliongeza kwamba maafisa wa polisi wamezidisha doria zao baada ya serikali kujenga kambi zaidi karibu na wakazi.

’’Mpango wa Nyumba Kumi, doria za polisi na Kuongezwa kwa kambi zaidi za polisi karibu na makazi zimechangia pakubwa kwa usalama kuimarika ndani ya Wodi ya Nairobi Kusini, Bi Waithera akaambia Taifa Leo.

You can share this post!

Mshukiwa wa mauaji azuiliwa siku 14 Juja

Wakazi wa Thika kunufaika na umeme mitaani