• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Dini potovu lasababisha maafa ya wanne

Dini potovu lasababisha maafa ya wanne

Na ALEX KALAMA

Watu wanne ambao ni wafuasi wa kanisa la Good News International, linalomilikiwa na mchungaji Paul Mackenzie wamethibitishwa kufariki eneo la Malindi baada ya kufunga kwa zaidi ya majuma mawili.

Akithibitisha visa hivyo, Afisa Mkuu wa

Idara ya Uchunguzi wa Jinai na Uhalifu (DCI) katika Kaunti Ndogo ya Malindi Bw Charles Kamau amesema wanne hao ni miongoni mwa watu 15 waliokolewa baada ya kupatikana wakiwa katika hali mahututi msitu wa Shakahola, ulioko kata ya Chakama.

Alhamisi, maafisa wa usalama walitumwa katika msitu huo kubaini ukweli wa tetesi za malalamishi yaliyotolewa kuhusu kufariki kwa wafuasi wa mhubiri Mackenzie kupitia hadaa zake.

Dini potovu la mchungaji huyo tata, inasemekana amekuwa akishawishi wafuasi wake kufunga bila kula, ili wafariki kuurithi ufalme wa mbinguni.

Kwenye kikao na wanahabari Mjini Malindi, Bw Kamau alidokeza kwamba maafisa wa polisi walifika katika vijiji kadhaa Shakahola na kufanikiniwa kuokoa watu 15.

Wanne kati yao, waliokuwa katika hali mahututi walifariki hata kabla kufikishwa hospitalini kupata matibabu.

“Tulipokea habari kuna watu wamelazimishwa kufunga hadi wakafa, ili waweze kukutana na Yesu,” alisema afisa huyo akitahadharisha umma kuhusu dini potovu ya mchungaji Mackenzie.

Baadhi ya wahanga wa dini potovu ya pasta Paul Mackenzie wa kanisa la Good News International waliookolewa na askari Malindi. PICHA / ALEX KALAMA

Wafuasi 11 waliosalia baada ya kuokolewa, wanaendelea kupokea matibabu Hospitalini Malindi.

Waumini 3 kati yao wako katika hali mbaya, huku idadi kamili ya waliofariki kutokana na dini hilo potovu ikikosa kujulikana.

Idara ya polisi Malindi inaendelea kufanya oparesheni kutafuta waliojificha vichakani, wakijinyima chakula na maji kufuatia hadaa za pasta Mackenzie.

Bw Kamau alidokeza kuwa polisi hawajafaulu kutambua makaburi yanayoaminika kuzikwa baadhi ya waumini, wakiwemo watoto jitihada za walinda usalama zikitatizwa na wakazi waliokuwa na ghadhabu.”Kwa mujibu wa taarifa tuliyopokea, inakadiriwa kuna makaburi 31 ya waumini wa Mackenzie, yaliyoko katika vichaka vya shamba analolimiki.”Majuma kadha yaliyopita, mhubiri huyo alishtakiwa mahakamani kwa tuhuma za kulazimisha wafuasi wake kujinyima chakula na maji.

Hata hivyo, aliachiliwa kwa dhamana.

 

  • Tags

You can share this post!

KIKOLEZO: Wazito waliojipanga

Zetech Sparks watuma onyo kwa Thika Queens Kombe la FKF

T L