• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Mbunge kushirikiana na serikali ya kaunti kuhamisha dampo

Mbunge kushirikiana na serikali ya kaunti kuhamisha dampo

NA ALEX KALAMA

MBUNGE wa Malindi Amina Mnyazi ameahidi kushirikiana na serikali ya Kaunti ya Kilifi ili kulihamisha jaa la taka la eneo la Timboni mjini humo ambalo limegeuka kero kwa wakazi.

Mbunge huyo amebainisha kuwa tayari amefanya mazungumzo na Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro ili kufanikisha mpango huo hivi karibuni.

“Suala la majaa ya taka huangaziwa na serikali ya kaunti lakini uzuri ni kwamba tumeshazungumza na gavana Gideon Mung’aro na yeye anajua yale matatizo ambayo sisi watu wa Malindi tunakumbana nayo,” alisema Bi Mnyazi.

Kiongozi huyo alieleza haja ya kupatikana kwa ardhi mbadala ya kutekeleza mpango huo kabla ya kuhamishwa kwa jaa hilo.

Aidha mbunge huyo alidokeza kuwa serikali ya kaunti ina ardhi ya kutosha katika eneobunge hilo ya kutumika kufanikisha mpango wa kuhamishwa kwa jaa hilo.

Mpango wa kuhamishwa kwa jaa hilo unajiri tu baada ya wakazi wanaoishi karibu na jaa hilo kuibua madai ya kwamba kuna uharibifu wa mazingira.

  • Tags

You can share this post!

Raila kujenga hoteli itakayogharimu nusu bilioni Malindi

CECIL ODONGO: Kwa kiongozi dikteta, mwisho wa ubaya ni aibu

T L