• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 12:59 PM
CECIL ODONGO: Kwa kiongozi dikteta, mwisho wa ubaya ni aibu

CECIL ODONGO: Kwa kiongozi dikteta, mwisho wa ubaya ni aibu

NA CECIL ODONGO

KUNA msemo kuwa anayetawala kwa mkono wa chuma naye hukumbana na kifo cha kikatili.

Msemo huu unatumiwa hasa kurejelea watawala ambao wananyanyasa na kuua raia wao.

Unawakumbusha kuwa, hata wao wataandamwa na mauti kwa njia hiyo hiyo.

Kote ulimwenguni viongozi wengi ambao waliishia kuwa madikteta, waliaga dunia katika upweke bila chochote.

Utajiri na mamlaka yao yaliyoyomea kama umande.

Wakati wa utawala wao walitumia nguvu za kijeshi na vyombo vya usalama kuua raia ambao walikuwa na maoni kinzani nao.

Walikamata na hata kuua viongozi waliopinga sera zao za uongozi, na pia kutumia mamlaka kuangamiza halaiki ya raia waliopinga dhuluma dhidi yao.

Baadhi ya madikteta ingawa hawakufariki mikononi mwa watesi wao, waliandamwa na maradhi sugu yasiyokuwa na tiba.

Wengine familia na jamaa zao waliishia kuwa wehu kwa sababu damu ya wale walioamuru wauawe iliwaandama maishani.

Miongoni mwa madikteta walioendeleza ukatili wa kuua raia na wapinzani ni aliyekuwa kiongozi wa Italia Bennitto Musolini, Adolf Hitler (Ujerumani), Francois ‘Papa Doc’ Duvalier (Haiti), Idi Amin (Uganda), Mae Zedong (China) na Muammar Gaddafi (Libya).

Duvalier alichaguliwa rais wa Haiti mnamo 1957 na mara moja akaanza kuonyesha ukatili kwa kunyanyasa wapinzani na raia.

Alitesa wapinzani na kufanya baadhi yao kukimbia uhamishoni ili kuepuka ghadhabu zake.

Duvalier aliamuru wafuasi wa wapinzani wauawe au kufungwa jela ili kuzima uasi wowote dhidi ya utawala wake.

Aliandamwa na ugonjwa wa moyo mnamo 1959. Ikaongeza kisukari pamoja na mengine sugu, akafa kifo kibaya 1979.

Katika taifa jirani la Uganda, Amin aliingia mamlakani 1976 kupitia mapinduzi ya kijeshi.

Aliua halaiki ya raia, na kuna simulizi ya kuatua moyo jinsi alihadaa walemavu kwamba angewasaidia lakini akawakusanya na kuwatumbukiza ziwa Victoria.

Amin alitorokea uhamishoni Jeddah, Saudia, mnamo 1979. Alifariki Agosti 2003 baada ya figo yake kuzimia na kufanya mwili wake uvimbe kama pipa.

Akazikwa huko uhamishoni wala si Uganda alikozaliwa.

Muammar Gadhafi pia ni kati ya viongozi ambao udikteta wao ulichosha raia wa Libya, ambao aliwaongoza kati ya 1969-2011.

Baada ya maasi kutanda alijificha shimoni akijaribu kutoroka taifa hilo.

Lakini akanaswa na majeshi ya Marekani ambayo yalisaidia kumtoa madarakani.

Alibururwa na waasi wakampiga risai kichwani kabla kufariki.

Vivyo hivyo, mwili wa Hitler na mkewe ulichomwa kwa asidi wakati wa kifo chao.

Siku za mwisho za uhai wake, Hitler alijutia sana ukatili aliofanya dhidi ya raia wa Ujerumani.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge kushirikiana na serikali ya kaunti kuhamisha dampo

Azimio wawaenzi waandamanaji waliouawa, kujeruhiwa na polisi

T L