• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 2:00 PM
Wafanyabiashara waomba taa irekebishwe sokoni Kisekini

Wafanyabiashara waomba taa irekebishwe sokoni Kisekini

NA SAMMY KIMATU

WAFANYABIASHARA katika kijiji cha Kisekini, kaunti ndogo ya Kathiani, Kaunti ya Machakos, wanakadiria hasara baada ya taa ya kituo cha kibiashara cha Kisekini kuharibika.

Kutokana na hali hiyo, wafanyabiashara wanalazimika kufunga biashara kabla ya saa moja usiku.

Akizungumza na Taifa Leo jana Jumatano, mhudumu wa duka, Bw Joseph Nzomo Kasema, alisema hawawezi kufanya biashara kwa saa nyingi usiku kwa sababu ya giza.

“Kabla ya taa kuharibika, tulikuwa tukiwahudumia wateja wetu hadi saa tano usiku lakini leo mambo hayaendi sawa kwa sababu taa ya sokoni imeharibika,” Bw Nzomo alisema.

Wazaki hao wameitaka serikali ya kaunti ya Machakos kushughulikia tatizo hilo ili kuwanasua wasipate hasara zaidi.

Vile vile kutokana na hali hiyo, wanasema ni hatari kwa usalama wa soko ikiwa giza litaendelea kushuhudiwa katika maduka na vibanda vyao usiku.

Tayari maduka mawili yamevunjwa na wezi wa mabavu ambao hawakukamatwa.

Mwenyekiti wa usalama katika eneo hilo, Bw Benson Him Nzyoki, alisema wakazi hulazimika kuwa chonjo nyakati za usiku wakihofia maduka kuvunjwa.

  • Tags

You can share this post!

Kamworor kutoana jasho na Mo Farah kwenye mbio za Great...

Uganda Airlines yalenga kuongeza safari zake Mombasa

T L