• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Wafanyakazi wa Pan Paper walilia haki

Wafanyakazi wa Pan Paper walilia haki

Na BRIAN OJAMAA

WAFANYAKAZI wa zamani kampuni ya karatasi Pan Paper Webuye ambaye sasa inaitwa Rai Paper Company, wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati ili walipwe malimbikizi ya mishahara ya kiwango cha Sh640 milioni.

Zaidi ya wafanyakazi 1,200 waliachishwa kazi mnamo 2009, wakati ambapo kampuni hiyo iliwekwa chini ya usimamizi wa mrasimu. Hii ni kufuatia usimamizi mbaya wa pesa na rasilimali nyingine za kampuni hiyo. Bw Francis Barasa Wakhungu, ambaye ni mwakilishi wao, alisema wengi wa wafanyakazi wa zamani wanaishi maisha ya uchochole baada ya kupoteza ajira.

Bw Barasa alisema mnamo Desemba 2016, wakati wa kufunguliwa upya kwa kiwanda hicho mjini Webuye, baada ya kununuliwa na kampuni ya Rai Group of Companies, Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kuwa wafanyakazi wa zamani wangelipwa.

Lakini tangu wakati huo mpaka sasa ahadi hiyo haijatimizwa. Bw Barasa alisema mnamo Agosti 2017, serikali ilitoa malipo ya wafanyakazi hao ya miezi mitatu. Hata hivyo, walilipwa asilimia 30 pekee ya mishahara yao ya kila mwezi. Bw Barasa ambaye aliajiriwa katika kampuni hiyo mnamo 1989 alisema waliachwa bila chochote cha kufanya kampuni hiyo ilipoporomoka.

Alisema juhudi zao za kutaka walipwe malimbikizi ya mishahara yao iligonga mwamba.

You can share this post!

Serikali yaruhusu wafanyabiashara kuagiza tani 577,000 za...

Idara ya Utabiri wa Anga yaonya kuhusu mafuriko

T L