• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Idara ya Utabiri wa Anga yaonya kuhusu mafuriko

Idara ya Utabiri wa Anga yaonya kuhusu mafuriko

Na KNA

IDARA ya Kutabiri Hali ya Anga katika Kaunti ya Kilifi imeonya kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa mafuriko huku vua fupi za msimu wa vuli zikinyesha kaunti hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga katika Kaunti hiyo, Getrude Leshamta, alitangaza Jumatano kuwa eneo hilo linapaswa kutarajia vua kubwa za msimu wa masika kuzuka ghafla lakini akasisitiza kwa msimu huo utakuwa mfupi wenye vua chache.

Alisema haya alipokuwa akihutubia mkutano wa Kamati ya Kaunti hiyo uliofanyika katika hoteli ya Kilifi. “Tumekuwa tukipata vipindi vya vua kubwa wakati mwingine na dhoruba nara kwa mara. Kwa sababu hiyo, tunatarajia mafuriko kuongezeka,” alisema katika mkutano huo.

Bi Leshamta alieleza kuwa kaunti hiyo inapitia vipindi visivyo vya kawaida vya hali ya anga ambapo misimu ya vua na kiangazi vinashuhudiwa kwa pamoja, akisema ni hali hatari kutokana na kwamba ni vigumu kuirabiri. Hali hiyo ya anga aliyoitaja kama La Nina inatarajiwa kuendelea hadi mwisho wa Januari lakini kiangazi kinatarajiwa kuendelea kuhangaisha eneo hilo kupitia dhoruba mpya.

“Sote tumeona barabara zikisombwa na watu kupoteza maisha kwa sababu ya vua kubwa zinazozuka ghafla ambapo kumekauka kisha ghafla kunanyesha na saa moja baadaye hakuna mvua hivyo watu wanavutiwa kutembea huku na kule,” alifafanua.

Kutokana na athari zake zinazotarajiwa, Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga imeshauri idara husika na wadau wengineo kutambulisha maeneo yanayoathiriwa zaidi na mafuriko na mikondo inayotumika kutuma msaada katika mipango yao ya uokoaji ili kujiandaa kwa matukio kama hayo kwa usalama wa watu.

Alihimiza Serikali ya Kaunti na wafadhili kutumia msimu huu wa vua fupi na kubwa zinazoshuhudiwa kaunti hiyo.

You can share this post!

Wafanyakazi wa Pan Paper walilia haki

Ganda la muwa la vigongo westham anayeng’aria Ajax

T L