• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 3:12 PM
Serikali yaruhusu wafanyabiashara kuagiza tani 577,000 za chakula cha mifugo

Serikali yaruhusu wafanyabiashara kuagiza tani 577,000 za chakula cha mifugo

Na WINNIE ONYANDO

SERIKALI imeruhusu kampuni 19 nchini kuagiza vyakula vya mifugo kutoka nchi za nnje.

Haya yanajiri miezi michache baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza ukame kama janga la Kitaifa. Kampuni hizo 19 zitaagiza mahindi yenye rangi ya manjano 225,950, maharagwe ya soya 184,550, mbegu ya pamba 20,500, mbegu ya alizetu 83,300, mtama wenye rangi nyeupe 34,000 na chakula cha samaki 28,750.

Miongoi mwa kampuni hizo ni Bidco Africa Limited, Farmers Choice Limited, Kitale Industries Limited, Mombasa Maize Millers Limited, Pembe Flour Mill Limited, Rift Valley Products Limited na kadhalika. Kwa jumla, Kenya sasa itaagiza chakula cha mifugo tani 577,052 huku hatua hiyo ikilenga kuimarisha sekta ya ufugaji nchini na kupunguza vifo vya mifugo.

“Vyakula hivyo vilianza kuagizwa Novemba, 31 na hatua hiyo itaendelea hadi Octoba, 31 mwaka wa 2022. Tunaamini kuwa hatua hiyo itapunguza vifo vya mifugo nchini na kuinua sekta hiyo,” ikasoma ripoti.Hata hivyo, serikali imetoa onyo kuwa mahindi yenye rangi ya manjano zitakazoagizwa kutoka nnje isiimarishwe kijenetiki na kutimiza matakwa ya shirika la kuthibiti viwango nchini(KBS).

“Vyakula vyote vya mifugo vitakavyoagizwa lazima yatimize masharti ya KBS. Hii itailinda mifugo yetu dhidi ya kemikali hatari. Vyakula hivyo vyote pia sharti viigizwe Octoba, 31 2022 au kabla ya hiyo tarehe,” ikasoma ripoti.

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Sudan hatarini kutekwa na jeshi kama Misri

Wafanyakazi wa Pan Paper walilia haki

T L