• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
Balala ashtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi

Balala ashtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi

NA PHILIP MUYANGA

ALIYEKUWA Waziri wa Utalii Najib Balala na Katibu Leah Gwiyo wameshtakiwa Ijumaa katika Mahakama ya Malindi kwa matumizi mabaya ya ofisi.

Wamefikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Malindi James Mwaniki ambapo wamekanusha mashtaka.

Kwa mujibu wa nakala ya mashtaka, wanadaiwa kutumia vibaya mamlaka yao kwa kuzipa kandarasi kampuni za Baseline Architects Ltd, Ujenzi Consultants, Armitech Consulting Engineering, na West Consult Consultant Engineers.

Hatua hiyo ilikiuka uamuzi wa Baraza la Mawaziri wakati huo ambapo wawili hao wanadaiwa kupuuza na kutafuta huduma kutoka sekta ya kibinafsi ambapo malipo yasiyofaa ya Sh3.3 bilioni yalielekezwa kwa kampuni hizo kwa huduma za mchoro wa mradi, kuandaa stakabadhi, kusimamia na kuendeleza mradi wa chuo cha Utalii cha Ronald Ngala.

Mshtakiwa mwingine ambaye ni Bw Joseph Odero akifanya kazi kama Westconsult Engineers amekanusha shtaka la kupokea kiharamu malipo ya Sh292.4 milioni kutoka kwa mfuko wa Tourism Fund ambayo awali ilifahamika kama Catering and Tourism Development Levy Trustees.

Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu kuachiliwa ama kwa bondi au dhamana ya pesa taslimu ifikapo saa tisa alasiri.

Upande wa mashtaka haukupinga washtakiwa wakiachiliwa kwa dhamana.

  • Tags

You can share this post!

Balala afikishwa mahakamani Malindi kwa kesi ya ufujaji...

Rais Ruto asambaza zawadi za Krismasi, wewe umefikiwa?

T L