• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
DPP aomba aliyetapeli wabunge nusu milioni asalie gerezani

DPP aomba aliyetapeli wabunge nusu milioni asalie gerezani

Na RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI Mkuu wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji ameomba mahakama imnyime dhamana mwanaume anayeshtakiwa kuwalaghai wabunge wawili Sh700, 000 katika uhalifu wa kimitandao.

DPP aliomba Boniface Kipchumba Kirui anayeshtakiwa kuwatapeli Mbunge wa Marakwet Magharibi Timothy Kipchumba Toroitich na Mbunge wa Matungulu, Stephen Mule azuiliwe katika gereza la Kamiti hadi kesi kadhaa zinazomkabili zisikizwe na kuamuliwa.

“Nimeamriwa na DPP niombe mahakama iamuru Kirui azuiliwe katika gereza la Kamiti hadi kesi zinazomkabili zikamilishwe. Mshtakiwa yuko na mazoea ya kurudia makosa haya haya akiwa nje kwa dhamana,” kiongozi wa mashtaka Judy Koech alisema.

Bi Koech alileza korti mshtakiwa anaendelea kuchunguzwa na asasi kadhaa za serikali kwa vile ni mmoja wa kundi la wahalifu wanaopora wananchi pesa kwa ulaghai wakitumia kadi za simu za Safaricom.

Kirui alishtakiwa kunyonya akaunti za Toroitich na Mule kwa kukopa mikopo na kuchukua pesa kutoka kwa akaunti zao.

Mbali na kuwalaghai pesa za akaunti zao, Kirui pia alitumia simu za wanasiasa hao kukopa pesa kutoka kwa makampuni mengine yanayotoa mikopo.

Hakimu alielezwa Kirui ni mmoja wa kundi la wahalifu wa kimitandao waliotapeli watu Bomet, akiwemo afisa mkuu wa polisi.

Kirui alikana mnamo Aprili12, 2023 alimlaghai Toroitich Sh547, 567.

Pesa hizi zilikung’utwa kutoka kwa akaunti yake iliyo katika benki ya Kenya Commercial Bank.

  • Tags

You can share this post!

Man-City pazuri kutinga fainali ya UEFA baada ya...

Idadi ya walioaga dunia Shakahola yagonga 150

T L