• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Mjakazi anayedaiwa kumuua afisa wa kaunti kuzuiliwa siku 14 zaidi

Mjakazi anayedaiwa kumuua afisa wa kaunti kuzuiliwa siku 14 zaidi

NA MAUREEN ONGALA

MJAKAZI Diana Naliaka anayetuhumiwa kumuua afisa wa serikali ya Kaunti ya Kilifi, atazuiliwa katika gereza la Malindi GK hadi Agosti 31, 2023.

Naliaka, almaarufu Sarah Nekesa Barasa au Diana Nanjala, amefikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama Kuu ya Malindi, Bw James Mwaniki, aliyeamua mshukiwa apelekwe gereza kuu la Malindi hadi Agosti 31, wakati ambapo atafanyiwa uchunguzi wa kiakili na pia kutafutiwa wakili wa kujitolea.

Naliaka, ambaye alikuwa mjakazi wa Rahab, anatarajiwa kushtakiwa kwa mauaji anayodaiwa alifanya mnamo Julai 20, nyumbani kwa mwajiri wake katika mtaa wa Mnarani Classic.

Mshukiwa atakabiliwa na shtaka la kumuua Afisa Mkuu wa Uchumi wa Baharini katika Serikali ya Kaunti ya Kilifi, Bi Rahab Amani Karisa katika nyumba yake ya kupanga iliyoko Govolani katika Mnarani Classic mnamo Julai 20, 2023.

Tangu kukamatwa kwake, Hakimu Mwandamizi Mkuu wa Kilifi Justus Kituku alikuwa ameagiza azuiliwe kwa siku 14.

  • Tags

You can share this post!

Bunge lahalalisha Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo

Tuwei achaguliwa naibu rais wa Shirikisho la Riadha Duniani

T L