• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 3:12 PM
Mshukiwa mkuu katika kashfa ya NYS kukamatwa

Mshukiwa mkuu katika kashfa ya NYS kukamatwa

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Jumanne iliamuru mmoja wa washukiwa wakuu katika kesi ya ufisadi uliokumba shirika la huduma ya vijana kwa taifa (NYS) ameamriwa akamatwe.

Bi Phylis Ngirita aliamriwa atiwe nguvuni na hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Bw Bernard Ochoi alipokosa kufika kortini wakati wa kusikizwa kwa kesi inayomkabili ya kukwepa kulipa ushuru wa Sh19milioni. Mbali na kuamuru Bi Ngirita atiwe nguvuni hakimu pia alimwagiza mdhamini aliyemlipia dhamana Phyilis afike kortini kueleza sababu za kutohakikisha mshtakiwa amefika kortini wakati wa kusikizwa kwa kesi.

Ombi mshtakiwa akamatwe liliwasilishwa na kiongozi wa mashtaka Bw James Gachoka. Akitoa uamuzi Bw Ochoi alisema: “Hii mahakama imetilia maanani ombi la kiongozi wa mashtaka Bi Ngirita akamatwe. Nakubaliana naye mshtakiwa amekosa kufika kortini. Naagiza polisi wamshike na kumfikisha kortini.”

Pia aliagiza mdhamini aliyemsimamia mshtakiwa kortini aachiliwe kwa dhamana afike kortini kueleza kilichojiri. Bi Ngirita anakabiliwa na mashtaka manne ya kukwepa kulipa ushuru. Shtaka lasema kuwa mnamo Desemba 31 20217 akifanya biashara kupitia kampuni ya Njewanga alikataa kulipa ushuru wa Sh13.7milioni.

Shtaka pili limesema alikosa kulipa ushuru wa Sh6.9milioni mnamo 2016. Alikanusha mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana.

Phylis Ngirita katika Mahakama ya Milimani…Picha/RICHARD MUNGUTI

You can share this post!

Mwanasoka anayelenga kufuata nyayo za Sergio Ramos wa PSG

Wanjigi alala ndani licha ya kujifungia usiku kucha

T L