• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 9:50 AM
Ndoa na familia za walimu sasa kuimarika

Ndoa na familia za walimu sasa kuimarika

NA MWANGI MUIRURI
SERA ya Wizara ya Elimu hapo mbeleni ilikuwa kwamba mwalimu angetumwa kufundisha katika shule za mbali kama njia moja kupigia debe uwiano wa kitaifa.

Baada ya walimu kuteta kwamba sera hiyo ilikuwa ikisambaratisha ndoa, pamoja na kuzua changamoto katika malezi ya watoto, serikali sasa imeizima.

Akizungumza Mjini Kenol, Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti kuhusu Elimu, Bw Joe Nyutu alisema kwamba hakuna mwalimu mkuu atakubaliwa kubagua wanafunzi kwa msingi wa sare.

“Hasa katika msingi wa dini, hakuna mwanafunzi atafukuzwa shuleni kwa kuvalia nguo zinazoambatana na imani za kidini.

“Ni furaha kuu kwamba leo Waziri Ezekiel Machogu ametuhakikishia kwamba sera ya kulazimisha walimu kuhudumu mbali na familia zao haitatekelezwa tena. Ni furaha kuu kusikia hayo na kupata hakikisho kwamba msingi wa dini utaheshimiwa na wanafunzi watakubaliwa kujipamba kwa itikadi zao za imani,” akasema Bw Nyutu.

Seneta huyo alielezea kwamba Waziri lazima ajitume kuhakikisha walimu wakuu hawatozi wazazi ada haramu na mwongozo wa karo uzingatiwe.

Alisema kuna ukora mwingi sana katika udhibiti wa ada shuleni, wazazi wakiendelea kutwikwa kila aina ya gharama haramu.

 

  • Tags

You can share this post!

Mbunge wa UDA apendekeza Raila aanze kupewa pesa za hazina...

William Kabogo akumbuka kanisa la alikozaliwa

T L