• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Portland sasa kuuza vipande vitatu vya ardhi yake ikiwapa kipaumbele wanaoishi humo

Portland sasa kuuza vipande vitatu vya ardhi yake ikiwapa kipaumbele wanaoishi humo

NA CHARLES WASONGA

KAMPUNI ya kutengeneza saruji ya East African Portland Cement Co. (EAPCC) sasa imetangaza kuwa inauza vipande vyake vitatu vya ardhi katika eneo la Mavoko huku ubomoaji ukiendelea katika ardhi yake yenye utata eneo hilo.

Kwenye tangazo katika magazeti ya Jumanne, Oktoba 17, 2023, kampuni hiyo inasema kuwa inauza vipande vya ardhi zenye nambari za usajili (LR no) 8784/144, 145 na 653 ambazo ziko karibu na Chuo Kikuu cha Daystar kando ya barabara ya Mombasa Road.

Kampuni hiyo inasema kuwa wakati wa uuzaji huo, kipaumbele kitapewa watu ambao wakati huu wanakalia sehemu za vipande husika vya ardhi.

EAPCC inawapa watu hao makataa ya siku 14 kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi hiyo kuwasilisha nia yao ya kutaka kununua ardhi husika.

“Kampuni ya EAPCC ingependa kujulisha umma kuhusu nia yake ya kuuza vipande vya ardhi vilivyotajwa hapo juu kwa njia ya urasimishwaji,” ikasema notisi hiyo iliyochapishwa kwenye magazeti ya ‘Daily Nation‘ na ‘Business Daily‘.

“Baada ya muda wa notisi hii kuisha, wanaozikalia ardhi hizi endapo hawatakuwa wameonyesha nia ya kuzinunua, zitauzwa kwa watu wenye haja,” inaongeza notisi hiyo.

Hata hivyo, ardhi hizo zinazouzwa sio sehemu ya ardhi tata ambako shughuli ya ubomoaji wa majumba ya makazi, shule na makanisa, inaendelea tangu Ijumaa wiki jana.

Ardhi hiyo tata ni ya ukubwa wa ekari 4,000 na yenye nambari ya usajili ya 10424.

  • Tags

You can share this post!

Kisii: Makanisa, wahubiri kuanza kulipa maelfu kuruhusiwa...

Timu ya chesi ya KCB tayari kwa mashindano ya...

T L