• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Timu ya chesi ya KCB tayari kwa mashindano ya ‘Mombasa Open’

Timu ya chesi ya KCB tayari kwa mashindano ya ‘Mombasa Open’

NA TOTO AREGE

TIMU ya chesi ya KCB inapania kufanya vizuri katika mashindano ya Mombasa Open Chess Championships yatakayofanyika Oktoba 20 hadi Oktoba 22, 2023, katika Mombasa Beach Hotel, Mombasa.

Kwenye mashindano hayo ambayo yatahusisha timu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, mshindi katika kitengo cha Open atajishindia Sh50,000 na mshindi wa upande wa wanawake anatarajiwa kuenda nyumbani na Sh20,000.

Mchezaji wa pili bora katika kitengo cha Open, atajishindia Sh30,000 wakati mchezaji wa pili upande wa wanawake atapokea Sh15,000.

Mchezaji wa pili bora katika kitengo cha chipukizi atapata medali ya fedha katika mashindano ambayo tayari yamevutia wachezaji 59.

KCB itakuwa chini ya uongozi wa Benjamin Magana akisaidiwa na magwiji wa Shirikisho la Chesi Duniani (FIDE) Martin Njoroge, Joyce Nyaruai, Bernard Nguku, na Robert McLigeyo.

Akizungumza wakati wa mazoezi katika KCB Club, Ruaraka jijini Nairobi, Meneja wa Timu Isaac Babu amesema wana hamu kubwa ya kushiriki katika Mombasa Open kwa sababu wanaamini kuwa wingi wa vipaji ndani ya kikosi cheo unawapa nguvu.

“Hiyo ni fursa inayotupa jukwaa bora la kujaribu uwezo wetu dhidi ya wachezaji bora wa chesi kutoka kanda ya Afrika Mashariki,” akasema Bw Babu.

Katika mashindano ya ligi ya chesi, KCB wanashikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali wakiwa na alama 33.

Equity wanafuata katika nafasi ya pili nao Nairobi Chess Club wakifunga tatu-bora na alama 31 na 29 mtawalia.

  • Tags

You can share this post!

Portland sasa kuuza vipande vitatu vya ardhi yake ikiwapa...

Wakazi 2,000 wa Kabati wafurika shuleni Mukerenju kwa...

T L