• Nairobi
  • Last Updated June 13th, 2024 6:05 PM
Rais Ruto amuomboleza Muthoni wa Kirima kama shujaa aliyetumikia taifa kwa kujitolea

Rais Ruto amuomboleza Muthoni wa Kirima kama shujaa aliyetumikia taifa kwa kujitolea

NA SAMMY KIMATU

RAIS William Ruto ameongoza Wakenya kumuomboleza shujaa wa vita vya uhuru ‘Field Marshal’ Muthoni wa Kirima aliyefariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 92.

Marehemu alikuwa katika mstari wa mbele kwenye vita vya ukombozi miaka ya 50 (1950s) wakati wa uhai wake.

Aidha, amefariki katika hospitali moja iliyoko katika mtaa wa Pangani, Nairobi

Rais Ruto amemtaja marehemu kama shujaa aliyechangia pakubwa vita vya uhuru wa Kenya kutoka kwa utawala wa ukoloni.

“Alikuwa jasiri, mchapakazi na aliipenda familia yake. Alitumikia jamii yake na kujitolea kwa ajili ya nchi yetu akiwa kwenye mstari wa mbele. Pumzika kwa amani Shujaa wetu,” Rais Ruto akaandika kwa mtandao wa Twitter.

Kadhalika, Naibu Rais Rigathi Gachagua amemuomboleza kwa kusema, “Naungana na familia yake na vizazi vya vita vya Ukombozi vya Maumau kuomboleza kifo cha Mama yetu, Shujaa Muthoni wa Kirima. Aliongoza wapiganaji wa Maumau baada ya kutekwa nyara kwa shujaa Dedan Kimathi ambaye alihudumu kama msaidizi wake wa kibinafsi, baada ya kusalitiwa na wenzake. Tunabaki kuwa na deni kwa mashujaa hao waliojitolea kuikomboa nchi yetu,” Bw Gachagua akasema.

Gavana wa Nyeri, Bw Mutahi Kahiga ametangaza jana kwamba serikali ya kitaifa na ile ya Kaunti ya Nyeri, kwa pamoja zitahakikisha kwamba mwili wa mwendazake umehifadhiwa kwa hadhi kuu katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee Funeral, Nairobi.

  • Tags

You can share this post!

Kioja Gachagua akimsalimu Raila baada ya kuapa awali...

Viongozi Mlima Kenya waendeleza uhasama dhidi ya wanahabari

T L