• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:25 PM
Serikali yatenga Sh130 milioni kupiga jeki kilimo cha miraa

Serikali yatenga Sh130 milioni kupiga jeki kilimo cha miraa

NA DAVID MUCHUI

SERIKALI imetenga Sh130 milioni kupiga jeki uzalishaji wa miraa.

Haya yamefichuliwa na Waziri wa Kilimo Mithika Linturi kwenye makala ya 55 ya Maonyesho ya Kilimo mjini Meru, aliyesema Ijumaa kwamba mgao huo utasaidia kuimarisha vyanzo vya maji na uboreshaji wa masoko katika maeneo ya ukuzaji wa miraa.

Ili kuhakikisha wakuzaji wanapata maji ya kutosha, waziri Linturi alisema pesa hizo zitatumika kujenga mabwawa ili yapatikane maji ya unyunyuziaji wa miraa.

Bw Linturi ameagiza Mamlaka ya Kilimo na Chakula (AFA) kushirikiana na Taasisi ya Miraa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Meru ili kuibuka na mikakati ya uongezaji thamani kwa miraa.

“Miraa ilileta pato la Sh6 bilioni mwaka 2022. Serikali imekuwa ikipiga jeki juhudi za uimarishaji wa zao la miraa tangu mwaka 2013 na hadi kufikia sasa, Sh344 milioni zimetumika kuimarisha vibanda vya miraa, vyanzo vya maji na uchimbaji mabwawa. Serikali ya Kenya Kwanza imejitolea kuhakikisha ukuzaji wa miraa unaimarika,” akasema Bw Linturi.

Mbali na kusaidia vyama viwili vya ushirika Meru na Embu kuwakinga wakulima wa miraa dhidi ya gharama ya juu ya uzalishaji, uimarishaji wa sera za miraa utasaidia pakubwa.

Waziri Linturi amesema ukuzaji wa miraa umepanuka maradufu tangu mwaka 2019 hadi 2023.

Mwenyekiti wa Muungano wa Wakuzaji wa Miraa wa Nyambene (Nyamita) Kimathi Munjuri amefurahia hatua ya serikali kutoa mgao kwa sekta ya miraa, akisema serikali ilikuwa imesitisha ufadhili mwaka 2020.

  • Tags

You can share this post!

Florence Diamond League: Chepng’etich afuta rekodi ya...

Watu wawili wafariki kwenye ajali ya matatu na trekta Ndhiwa

T L