• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 7:50 AM
Wakenya washerehekea Krismasi sehemu mbalimbali

Wakenya washerehekea Krismasi sehemu mbalimbali

Na WAANDISHI WETU

WAKENYA katika maeneo mbalimbali walikusanyika jana katika sehemu tofauti tofauti za burudani na maeneo ya kijamii kusherehekea sikukuu ya Krismasi.

Katika kila kaunti, tamasha hizo zilisherehekewa kwa njia mbalimbali kama njia ya kukumbuka kuzaliwa kwa Mwokozi.

Katika Kaunti ya Nairobi, tamasha hizo hazikuvurugwa na ujenzi unaoendelea katika eneo la Kijamii la Uhuru Park.

Sherehe hizo zilifanyika nje ya Uhuru Park huku wafanyabiashara wakifurahia idadi kubwa ya watu waliohudhuria eneo hilo kupata huduma mbalimbali kutoka kwao kama njia ya kusherehekea na watoto wao.

Katika eneo la Pwani, wageni na wakazi walikusanyika katika Ufuo wa umma wa Jomo Kenyatta, Mama Ngina Water Front, Fort Jesus na fuo za kibinafsi katika bahari ya Hindi kusherehekea Krismasi katika maeneo hayo.

Tofauti na mwaka 2020 wakati fukwe zilikuwa na idadi ndogo ya watu kwa sababu ya hatua kali za kuthibiti kusambaa kwa virusi vya corona, maeneo ya kijamii yalikuwa yamejaa watu kutoka mashambani na wenyeji.

Kasisi Nelson Barasa ni miongoni mwa waliosafiri na familia yake kutoka kaunti ya Bungoma kufurahia sherehe hizo Mombasa. Alisema hangeweza kuja kukaribisha mwaka wa 2021 kwa sababu ya vizuizi vya kusafiri vilivyowekwa wakati huo.

“Nilitaka kuvuka mwaka wa 2021 hapa Mombasa lakini hilo halikuwezekana. Hata hivyo, wakati huu fursa ilipatikana na tukaamua kusafiri,” akasema Bw Barasa.

Kwingineko, serikali ya Kaunti ya Kisumu iliandaa sherehe hizo barabarani huku mamia wakihudhuria tamasha hizo.

Katika Kaunti ya Kakamega, waumini katika kanisa la God faithful Mahondo walisherehekea Krismasi yao kwa kuwapa ubatizo waumini zaidi ya 5,000 katika mto Muyukwe, barabara ya Kakamega-Mumias.

BRIAN OCHARO, CECE SIAGO na WINNIE ONYANDO 

  • Tags

You can share this post!

Mswada tata wa vyama kujadiliwa Jumatano

TAHARIRI: Wakenya hawajaona zawadi ya stima nafuu

T L