• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:50 AM
Afueni ya muda kwa Zuma, korti ikiahirisha kesi

Afueni ya muda kwa Zuma, korti ikiahirisha kesi

Na MASHIRIKA

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

KWA mara nyingi mahakama moja nchini Afrika Kusini iliahirisha kusikizwa kwa kesi ya ufisadi inayomkabili aliyekuwa rais wa nchi hiyo Jacob Zuma hadi Septemba 9 kufuatia kulazwa hospitalini kwa kiongozi huyo wiki jana.

Zuma, aliyefungwa gerezani mwezi jana kwa kukaidi agizo la kufika mahakamani, hatua iliyosababisha fujo, alitarajiwa kufika mbele ya Mahakama Kuu ya Pietermaritzburge, Jumanne kuhusiana na kesi ya sakata ya ununuzi wa silaha iliyotokea alipohudumu kama naibu rais wa Afrika Kusini.

Sakata hiyo ya Dola 2 bilioni (Sh200 bilioni) ilisababisha kufutwa kwake mnamo mwaka wa 2005.Zuma, 79, anatumikia kifungo cha miezi 15 katika gereza la Estcourt lililoko mkoa wa KwaZulu-Natal, anakotoka.

Alipewa hukumu hii baada ya kidinda kuhudhuria kikao cha mahakama iliyokuwa ikiendesha kesi dhidi yake.Mnamo Ijumaa wiki jana alilazwa hospitalini kwa ukaguzi wa kimatibabu.

Jaji wa Mahakama Kuu Piet Koen jana alikubali ombi la mawakili wa Zuma kwamba kesi hiyo iahirishwe.Lakini jaji huyo aliamuru mawakili wa Zuma watoe ripoti kuhusu hali yake ya afya Agosti 20.

Vilevile, jaji Koen aliagiza serikali iteue daktari achunguze iwapo hali ya kiafya ya Zuma itamwezesha kushtakiwa.

Zuma anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi, utakasaji wa pesa na kukwepa kulipa ushuru wakati wa ununuzi wa silaha kuanzia miaka ya tisini (1990s).

Mnamo Mei 2021, kiongozi huyo wa zamani alikana mashtaka hayo.

You can share this post!

TAHARIRI: Ibainishwe mbona chanjo inakataliwa

Messi sasa mali rasmi ya PSG baada ya kutia saini mkataba...