• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Biden asifu uteuzi wa Rishi Sunak kuwa Waziri Mkuu

Biden asifu uteuzi wa Rishi Sunak kuwa Waziri Mkuu

LONDON, UINGEREZA

NA MASHIRIKA

RAIS wa Amerika, Joe Biden amesifu uteuzi wa Rishi Sunak, akisema ni hatua ya kimsingi inayolenga kuleta mabadiliko ulimwenguni.

Alisema Sunak ndiye Waziri Mkuu wa kwanza wa Uingereza ambaye sio mzungu. Biden anatarajiwa kumpongeza rasmi kiongozi huyo ambaye ana asili ya India na ambaye babake alizaliwa Kenya na mamake Tanganyika.

Kiongozi huyo mpya alikutana na Mfalme Charles III Jumanne ili kupata idhini ya kuunda serikali.

Sunak, alipata uungwaji mkono kutoka kwa wabunge wa Chama cha Conservative, kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo, baada ya Liz Truss aliyekuwa akishikilia kiti hicho kujiuzulu.

Sunak atakuwa waziri mkuu wa tatu wa Uingereza ndani ya muda wa wiki saba, baada ya kipindi cha machafuko ya kisiasa ambayo yameathiri nchi mbalimbali.

Huku mfumuko wa bei za bidhaa ukiwa zaidi ya asilimia 10 na uchumi ukitabiriwa kudorora, huenda mapumziko ya kisiasa ya Sunak yatakuwa mafupi.

Sunak alitoa hotuba fupi kwenye televisheni Jumatatu kutoka makao makuu ya Chama cha Conservative jijini London.
Kwenye hotuba yake, Sunak alitoa wito serikali za nchi mbalimbali kushirikiana ili kufufua uchumi.

“Uingereza ni nchi nzuri mno. Hata hivyo, tunakabiliwa na changamoto kubwa ya kiuchumi. Sasa tunahitaji utulivu na umoja,” alisema Sunak katika hotuba yake.

“Kuunganisha chama chetu na nchi yetu ni jambo la kimsingi kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee ya kupambana na changamoto zinazotukabili na kujenga mustakabali bora wenye mafanikio,” akasema Sunak.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Mauaji ya mwanahabari wa Pakistan nchini...

ZARAA: Siri yake ni bidii shambani na kusaka wateja...

T L