• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
WANDERI KAMAU: Mauaji ya mwanahabari wa Pakistan nchini yameipaka tope Kenya kimataifa

WANDERI KAMAU: Mauaji ya mwanahabari wa Pakistan nchini yameipaka tope Kenya kimataifa

NA WANDERI KAMAU

MAUAJI tata ya mwanahabari maarufu wa Pakistan, Arshad Sharif, katika eneo la Kajiado yameipaka tope Kenya kimataifa kama nchi isiyo salama kwa waandishi habari.

Kwa miaka mingi, Kenya imekuwa ikiorodheshwa kuwa miongoni mwa mataifa yanayozingatia usalama na uhuru wa wanahabari.

Hata hivyo, hali hiyo imekuwa ikibadilika katika siku za hivi karibuni kutokana na vitisho ambavyo vimeelekezewa wanahabari na watetezi wa haki za umma.

Mwanahabari Sharif si wa kwanza kuuawa kikatili na vikosi vyetu vya usalama.

Tangu mwaka 1990, makumi ya wanahabari, mawakili, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu wameangamizwa katika hali tatanishi, kwa kuonekana kuzikosoa serikali zilizo mamlakani.

Kufikia sasa, baadhi ya wanahabari na watetezi wa umma waliouawa katika mazingira tata ni mwanahabari Francis Nyaruri, mwanaharakati Oscar Kamau King’ara, wakili Willie Kimani kati ya wengine wengi.

Cha kushangaza ni kuwa, vifo vya watu hao vimebaki kuwa fumbo lisilo na jibu hadi sasa.

Vimebaki kuwa siri kuu iliyofichika katika nyoyo za wale waliopanga na kutekeleza mauaji hayo.

Katika kauli zake za mwanzo baada ya kutangazwa mshindi wa kura ya Agosti 9, Rais William Ruto aliahidi kutolipiza kisasi dhidi ya yeyote aliyekuwa akiupinga mrengo wake wa Kenya Kwanza, wakiwemo wanahabari.

Changamoto kuu kwa Rais Ruto ni kuhakikisha kuwa, mauaji hayo hayairejeshi Kenya katika enzi za giza; kama inavyoshuhudiwa katika baadhi ya nchi zinazokumbwa na mapigano yasiyoisha barani Afrika na kwingineko duniani.

  • Tags

You can share this post!

CECIL ODONGO: Miguna hatoshi kumbandua Raila ubabe wa siasa...

Biden asifu uteuzi wa Rishi Sunak kuwa Waziri Mkuu

T L