• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 6:36 PM
Madhehebu yenye itikadi kali yamewahi kuua wengi kimataifa

Madhehebu yenye itikadi kali yamewahi kuua wengi kimataifa

NA MASHIRIKA

HUKU idadi ya miili iliyofukuliwa Shakahola, Kaunti ya Kilifi, ikiendelea kuongezeka, matukio ambapo waumini hushawishiwa kujiua yamewahi kutokea kwingineko duniani.

Mbali na makundi ya kigaidi ambayo husemekana kuwashawishi washambulizi wa kujitolea mhanga kwamba, watapata mabikira mbinguni, matukio mengine yaliyotetemesha dunia ni kama yafuatayo:

1978, Guyana: Watu 914 kutoka Amerika walifariki katika kisa cha mauaji ya halaiki, baada ya mhubiri Jim Jones, kuwashauri wazazi kuwapa wanao sumu.

Mhubiri huyo aliwahamisha wafuasi wake kutoka San Francisco hadi Guyana, Amerika Kusini ili kukwepa taasisi za kiusalama. Alipatikana amefariki na jeraha la risasi kichwani.

2000, Uganda: Watu 700 wanaohusishwa na kundi lenye mafunzo potofu waliuwawa Kanungu, magharibi mwa Uganda kwa kuchomwa moto ndani ya kanisa lao.

Viongozi wa dini hiyo potovu hawakuwahi kupatikana.

1993, Texas: Watu 76 Texas, Amerika, waliaga dunia katika makabiliano na polisi walipovamia majengo yao ambayo yalikuwa yametengenezwa kwa mbao. Kati yao kulikuwa na watoto 20. Bw Branch Davidian, kiongozi wa dini hiyo, alishtakiwa kwa kukusanya silaha ambazo zilisababisha makabiliano makali ya siku 51 kati ya wafuasi wake na vikosi vya ulinzi.

1994, Canada: Watu 70 wa ‘kanisa la mwisho wa dunia’ nchini Canada wakiwemo viongozi wake, waliaga dunia. Inaaminika wengine wao waliuawa, wakitarajia dunia kuisha.

  • Tags

You can share this post!

Jubilee, KUP hawana mkataba na muungano wa Kenya Kwanza...

Kontena kutumika kuhifadhi miili baada ya mochari kujaa

T L