• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 6:30 PM
Rais Museveni athibitisha kuugua corona

Rais Museveni athibitisha kuugua corona

NA SAMMY WAWERU

RAIS wa nchi jirani ya Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuugua virusi vya corona.

Kupitia taarifa kwenye akaunti yake halisi ya Twitter, Bw Museveni alisema Alhamisi, Juni 8, 2023 aliambukizwa Homa hatari ya Corona akiwa kwenye shughuli kuhudumia nchi yake jijini Kampala.

Alianza kushuhudia dalili mnamo Jumanne, Juni 6, 2023 japo akapuuza akidhania ni homa au mafua tu ya kawaida wakati akishiriki mkutano Entebbe.

“Jumatano asubuhi, Juni 7, 2023 dalili hizo zilizidi ndiposa nikaita madaktari wangu waliofanya vipimo vitatu. Viwili viliashiria nilikuwa salama, na kimoja kikiashiria huenda nikawa na virusi vya corona,” Rais Museveni alielezea kupitia taarifa yake Twitter.

Ili kukinga familia yake isiambukizwe, anadokeza alisafiri kuelekea Kololo kwa kutumia gari la kipekee bila kuandamana na mkewe, Bi Janet Museveni.

Kololo, Bw Museveni alithibitishwa kamilifu anaugua ugonjwa wa Covid-19.

Kwa sasa, anaendelea kujitenga eneo la Nakasero huku akiendelea kupata matibabu.

Alitangaza kwamba amemtwika Waziri Mkuu Robinah Nabanjja majukumu yake ya Alhamisi, Juni 8, 2023 na Ijumaa, Juni 9, 2023.

Janga la Covid-19, lilitua Afrika Mashariki, Kenya ikiwemo Machi 2020.

  • Tags

You can share this post!

West Ham wakomoa Fiorentina na kufuzu kwa soka ya Europa...

Wahudumu wawili wa bodaboda wafariki baada ya kugongwa na...

T L