• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Wanaume hawawezi kustahimili habari mbaya kama wanawake – Utafiti

Wanaume hawawezi kustahimili habari mbaya kama wanawake – Utafiti

NA CECIL ODONGO

Wanaume hubana habari mbaya zinazowahusu na za watu wengine, watafiti wamebaini.

Utafiti huo ulioendeshwa na Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon Marekani unasema kuwa wanawake nao huwa na mazoea ya kueneza habari mbaya upesi mno.

Utafiti huo unasema kuwa wanaume wengi hubana habari mbaya kutokana na maumbile yao ambapo wao hushughulishwa na jinsi ambavyo habari hizo zitakavyochukuliwa na wanaozipokea.

Hata hivyo, wao huwa radhi kuzungumzia kuhusu habari nzuri zinazowahusu au zile zinazowahusu watu wengine bila kufichua mengi. Mara nyingi wanaume huwa vigumu kufichua mabaya yanayowakumba kwa sababu ya hofu kuwa nao maelezo yao yakigunduliwa, yataenezwa pia.

“Matokeo ya utafiti wetu ulionyesha kuwa kuna tofauti kati wanaume na wanawake kuhusu jinsi wanavyotoa na kupokea au kueneza habari nzuri na habari mbaya. Matokeo haya yanawasawiri wanaume kama wanaobana habari mbaya na hata hawana haraka ya kueleza habari zao nzuri,” ikasema utafiti huo.

Utafiti huo ulipigwa jeki na matumizi ya mitandao ya kijamii enzi hizi za utandawazi ambapo wanaume na wanawake hutumia mitandao kueneza habari kuhusu masuala mbalimbali.

Wanaume huwa na sababu maalum ya kufunguka kuhusu maelezo yao ya kibinafsi, iwapo ni habari mbaya na wanahisi zitapokelewa vibaya na familia zao. Wanawake nao huridhika sana wakieneza habari iwe mbaya au nzuri kwa sababu hawashughulishwi sana na jinsi ambavyo zitapokelewa.

“Wanaume hutathmini sana iwapo hatua ya kueneza habari hizo italeta matokeo hasi au chanya,” ikaongeza utafiti huo.

Wengi wa wanawake hujutia hatua ya kueneza habari mbaya kuhusu mtu baada ya kutazama athari yake, jambo ambalo hawalizingatii kabla ya kuzieneza.

  • Tags

You can share this post!

Majambazi wavamia makazi ya MCA Kisii usiku kukinyesha,...

DONDOO: Ndoa yadumu wiki 2 tu demu akidai jembe la mume ni...

T L