• Nairobi
  • Last Updated December 8th, 2023 10:25 PM
Akothee na mumewe, fungate yapamba moto

Akothee na mumewe, fungate yapamba moto

NA SAMMY WAWERU

MAPENZI motomoto yameendelea kusheheni kati ya mwanamuziki Esther Akoth ‘Akothee’ na mumewe Dennis Schweitzer.

Akothee alisafiri Juni 2023 Ugiriki, kwa minajili ya fungate.

Akitoa tangazo hilo kwa wafuasi wake kupitia akaunti zake za mitandao ya kijanii, msanii huyo alisema anaenda kufurahia fungate na mumewe mzungu aliyempa jina la utani ‘Omosh’.

“Kwaherini, @BwOmosh ameagizia mkewe. Ninapenda kuwa kwenye ndoa,” alichapisha katika ukurasa wake rasmi wa Facebook.

Kilichozua ucheshi zaidi mitandaoni, ni kudai anaenda kutafuta mimba.

“Ninaelekea fungate, mimba hiyo,” alielezea.

Wawili hao walifunga pingu za maisha mnamo Aprili 10, 2023 katika harusi iliyohudhuriwa na baadhi ya watu mashuhuri katika ulingo wa muziki, waigizaji, viongozi wa kisiasa na hata waziri katika serikali ya Rais William Ruto.

Kufuatia machapisho ya hivi punde, Akothee na kipenzi chake cha moyo wanaonekana kufurahia fungate.

Juni 2, 2023, mama huyo wa watoto watano alipakia video kwenye kurasa zake za Tiktok na Facebook wakikaribishwa katika hoteli ya kifahari Ugiriki.

Kwenye video hiyo, wanakaribishwa hotelini, mapenzi yakionekana kunoga na kupamba moto.

Wanandoa hao, wanatembea kwa madaha wakishikana viuno.

“Karibuni, mmefika kwa hoteli bora,” aliyenasa video hiyo anaskika akisema.

“Wanandoa wazuri katika eneo maridadi, fungate, ninawatakia kila la heri. Mfurahie.”

Atkothee, alifichua kwamba amekuwa Ugiriki zaidi ya siku saba kwa minajili ya fungate, na tofauti kati ya nchi hiyo na Kenya kibiashara ni mikakati maalum iliyowekwa kuivumisha.

“Wanachukua biashara kwa makini na kuitilia maanani, ninashangaa ni nani anayevumisha Kenya katika ngazi ya kimataifa kuifanya iwe bora hata kwa fungate?” akahoji staa huyo wa kibao maarufu cha ‘Kula Ngoma’.

Hata hivyo, Akothee anakiri taswira kimazingira na vivutio vya utalii Kenya inaongoza kinachokosekana kikiwa mikakati kuivumisha ng’ambo.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Musalia afunika Gachagua

Wandayi: Tutavuruga usomaji bajeti

T L