• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Amejipata tajiri kwa kuwashonea wateja nguo kwa ustadi mkuu

Amejipata tajiri kwa kuwashonea wateja nguo kwa ustadi mkuu

Na MAGDALENE WANJA

Bi Joan Aoko alikuwa na hamu kubwa ya kupata ajira baada ya kukamilisha masomo yake katika chuo kikuu ili kujipatia riziki. Alikuwa amefuzu katika kozi ya International Relations and Diplomacy with IT kutoka Chuo Kikuu cha Maseno.

Aliweza kupata kazi katika shirika lisilo la kiserikali na baadaye katika serikali ya Kaunti ambako alifanya kazi yake kwa bidii hadi mwaka 2017.

Ata hivyo, Jambo moja lilimfanya Bi Aoko kuwa tofauti na wenzake kazini. Alipenda Sana kushona kwa kutumia sindano ya mkono, jambo am also alifanya wakati wa ziada kama vile saa za mankuli.

Katika kazi zote mbili alipokuwa katika ajira, alikuwa na wateja ambao aliwauzia bidhaa alizotengeneza. Hii ilimuwezesha kujipatia pesa za ziada kando na mshahara wake.

Wakati mkataba wake na serika ya kaunti ulipofika mwisho, aliamua kutorudi kwenye ajira tena, na badala yake kufanya kazi ya ushonaji akiwa nyumbani kwake.

“Mteja wangu wa kwanza alinipa kazi ya kumshonea viatu vya mtoto wake na alinilipa Sh 1,000. Ni furahi sana na hii ilinitia moyo,” alisema Bi Aoko.

Ingawa Bi Aoko anasema kuwa hakuweza kuwasiliana tena na mteja huyo, anasema kuwa alikuwa kama Baraka katika biashara yake.

“Aliniambia kuwa nikifanya kazi hii kwa bidii, itanifikisha mbali katika maisha yangu,” aliongeza Bi Aoko.

Safari yake ya ushonaji alia za, alipokuwa mdogo baada kufunzwa na marehemu mamake ika hakujua angeifanya kama biashara.

“Ingawa, kazi zangu za kwanza haikuwa za kiwango cha Hali ya juu, niliendelea kuimarisha kazi yangu baada ya kupata wateja wengi zaidi,” alisema Bi Aoko.

Moja wapo ya kazi ambazo Bi Aoko anajivunia ni kuweza kujishonea rinda alilovaa katika harusi yake.

“Sikutaka kuwa na vazi la kawaida katika harusi yangu na Ndio sababu nilichukua muda kuitengeza nguo hio nilioivalia katika siku hio muhimu maishani mwangu,” aliongeza Bi Aoko.

Kufikia sasa, Bi Aoko ameweza kujipatia wateja wengi ambao huwashonea nguo za harusi, nguo za kuogelea, rinda na mavazi mengine ya kawaida kwa kutumia uzi.

Mojawapo ya gauni za harusi anazoshona dada huyu/MAGDALENE WANJA

Bi Aoko hushona nguo za kuogelea kwa Sh5,000 huku rinda akiuza Sh 7,500. Wale ambao hupenda kuvalia nguo ya harusi iliyoshomwa kwa uzi hulipwa Sh45,000.

Wengi wa wateja wake hupendakuvalia nguo hizo katika karamu au sherehe mbali mbali. Wengine huenda kununua sina hii ya mavazi ili kupeana kama zawadi katika sherehe kama vile siku ya kusherehekea siku ya kuzaliwa.

Alisema kuwa kinyume na nguo zingine za kawaida, aina hii ya mavazi hufanya mtu kuwa tofauti na kumfanyia ahisi vyema.“Mteja anaweza kuchagua rangi na muundo utakaomridhisha,” aliongeza.

Ata ivo, kazi hii Ina changamoto zake ambazo ni pamoja na muda mingi kutumika kabla kukamilisha aina yoyote ya kazi. “Kinyume na ushonaji wa kawaida ambao mashine hutumika, hii hutegemea mikono ambayo huchosha sana,” alisema Bi Aoko.

Ameweza kuwaajiri watu watatu ambao humsaidia katika kazi hio.

You can share this post!

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Duniani yathibitisha Kenya...

Kilimo bila kemikali kinalipa, Sylvia asimulia