• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:15 PM
Marioo asema ameshapata Sh6 milioni za kumuoa Paula Kajala

Marioo asema ameshapata Sh6 milioni za kumuoa Paula Kajala

Na SINDA MATIKO

MWANAMUZIKI staa Marioo kakiri kwamba yupo tayari kulipa mahari ya Tsh100 milioni (Ksh6 milioni) kwa demu wake soshiolaiti Paula Kajala.

Penzi la wawili hao kwa sasa limefikia patamu ikiwa ni miezi saba toka walipoanza kudeti.

Akifanya mahojiano hivi majuzi na runinga ya East Africa TV, Marioo alikiri kukoshwa na Paula kiasi cha kuwa tayari kumlipia kiasi hicho kama mahari.

Paulah ni binti ya produsa maarufu na mkongwe P Funk Majani pamoja na mwigizaji soshiolaiti Fridah Kajala.

Binti yao huyo aliwahi kuwa kwenye mahusiano na mwanamuziki Rayvanny. kabla ya kuwa na Marioo wake.

***

Wema ajibu wasiwasi wa mamake

Mahusiano ya mwigizaji modo Wema Sepetu na mamake mzazi Mariam Sepetu yanazidi kwenda vyongo.

Wawili hao wameendelea kupapurana hadharani. Ugomvi wao ulizuka baada ya Mariam kuonyesha kutoridhishwa na maamuzi ya bintiye kutoka kimapenzi na mwanamuziki Whozu.

Mariam alikiri wazi kwamba alihisi kudhalilishwa na binti yake kwa yeye na Whozu kuweka wazi mahusiano yao pasi na kumfahamisha ili aweze kutoa baraka zake.

Mfululizo wa ugomvi wao uliendelea baada ya modo wa zamani Jokate Mwegelo kupewa cheo juzi kati kusimamia idara ya vijana kwenye chama tawala nchini Tanzania CCM. Jambo hilolilionekana kumgusa mamake na kumtaka binti yake aanze kuwaza.

“Kama Jokate anajitambua, wakati wa Wema bado. Na Wema anatakiwa ajitambue na atafika mbali bado yeye ni kijana. ni mdogo,” Mariam alisema na wanahabari hivi majuzi kwenye mkutano wa CCM.

Ni matamshi yaliyoonekana kumkera Wema na akaamua kujibu.

“Mimi nitaambia watu, fanya kile kinachokupa wewe furaha. Ishi vile utakavyo wewe ilmuradi haileti drama. Maisha ni mafupi kuyaishi kwa ajili ya kumfurahisha mtu mwingine na sio wewe. Halafu pia kupangiana maisha sio kitu kizuri.”

 

***

Anita Nderu afichua siri ya ndoa

MWANAHABARI maarufu Anita Nderu amefichua siri ya ndoa yake ya miaka miwili kuwa juu ya kistari.

Kulingana na Nderu, watu wengi hukosea kwenye kumsaka mtu wanayedhamiria kudumu nao kwenye maisha haya.

“Usimtafute mtu aliyekamilika, badala yake mtafute mtu anayekukamilisha wewe. Pili, ni muhimu muwe na mtazamo sawa kwenye vitu vingi tu hivyo mtaepuka kukinzana kwa sababu maamuzi yatakuwa ni rahisi,” Anita anasema.

Mrembo huyo alifunga ndoa na mume wake mzungu Barret Raftery Septemba 2021, baada ya mwaka moja ya kudeti.

Penzi hilo liliota ikiwa ni baada ya Anita kuachana na mpenzi wake Sunny mnamo 2019, baada ya kudeti kwa miaka saba.


  • Tags

You can share this post!

Tineja akiri kuua afisa mkuu wa fedha wa Nairobi Hospital,...

Aliyevuruga mkutano wa Ruto atozwa faini ya Sh13,000

T L