• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 8:55 PM
BORESHA AFYA: Fahamu umuhimu wa cheri

BORESHA AFYA: Fahamu umuhimu wa cheri

MA MARGARET MAINA

[email protected]

CHERI ni matunda yanayopendwa zaidi na kwa sababu nzuri. Ni matamu na husheheni vitamini, na madini.

Virutubisho

Cheri ni matunda madogo ambayo huja katika rangi mbalimbali na ladha. Kuna aina mbili kuu.

Rangi zao zinaweza kutofautiana kutoka njano hadi nyeusi-nyekundu.

Yana kalori, protini,wanga,nyuzinyuzi, vitamini C, potasiamu, na manganisi.

Virutubisho hivi, hasa nyuzinyuzi, vitamini C, na potasiamu, hunufaisha afya kwa njia nyingi.

Vitamini C ni muhimu kwa kudumisha mfumo wako wa kinga na afya ya ngozi wakati potasiamu inahitajika kwa kusinyaa kwa misuli, utendakazi wa neva, udhibiti wa shinikizo la damu, na michakato mingine mingi muhimu ya mwili.

Cheri pia ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi, ambayo husaidia kuweka mfumo wako wa usagaji chakula kuwa na afya kwa kuchochea bakteria wa manufaa ya utumbo.

Kuongeza ahueni ya mazoezi

Cheri inaweza kusaidia kupunguza maumivu ya misuli yanayosababishwa na mazoezi, kama kuvimba. Shurubati ya cheri inaweza kuharakisha kupona kwa misuli, kupunguza maumivu ya misuli yanayosababishwa na mazoezi, na kuzuia kupoteza nguvu kwa wanariadha mashuhuri, kama vile waendeshaji wa baiskeli na wakimbiaji wa mbio za masafa marefu.

Kuimarisha afya ya moyo

Kuongeza ulaji wako wa matunda yenye virutubishi kama cheri ni njia nzuri ya kulinda afya ya moyo wako. Lishe yenye matunda mengi huhusishwa na kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo.

Cheri ni ya manufaa hasa katika suala hili, kwa kuwa ina virutubisho vingi na misombo ambayo inajulikana kukuza afya ya moyo, ikiwa ni pamoja na potasiamu, madini ambayo ni muhimu kwa kudumisha afya ya moyo wako.

Inahitajika kudumisha mapigo ya moyo ya kawaida na husaidia kuondoa sodiamu ya ziada kutoka kwa mwili wako, kudhibiti shinikizo la damu yako.

Ndiyo maana ulaji mwingi wa potasiamu umehusishwa na kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi.

Kukabili ugonjwa wa yabisi na ugonjwa wa jongo

Kwa sababu ya athari zake nyingi za kuzuia uchochezi, cheri zinaweza kupunguza dalili za ugonjwa wa yabisi na jongo, aina ya ugonjwa wa yabisi unaosababishwa na mkusanyiko wa asidi ya mkojo ambayo inaweza kusababisha uvimbe mkubwa na maumivu kwenye viungo vyako.

Cheri husaidia kukabili uvimbe kwa kukandamiza protini za uchochezi, ambazo zinaweza kusaidia kupunguza dalili zinazohusiana na ugonjwa wa yabisi.

  • Tags

You can share this post!

BORESHA AFYA: Vitamu visivyoleta madhara mwilini

Makabiliano Sudan watu zaidi ya 50 wakiuawa

T L