• Nairobi
  • Last Updated May 15th, 2024 8:55 PM
Dalili za upungufu wa iodini mwilini

Dalili za upungufu wa iodini mwilini

NA MARGARET MAINA

[email protected]

IODINI ni madini muhimu ambayo hupatikana katika samaki wa baharini.

Tezi ya binadamu huitumia iodini kutengeneza homoni za tezi, ambazo husaidia kudhibiti ukuaji, kurekebisha seli zilizoharibiwa na kusaidia michakato ya kimetaboliki .

Kwa bahati mbaya, watu duniani kote wako katika hatari ya upungufu wa iodini.

Walio katika hatari kubwa zaidi ni pamoja:

–         Wanawake wajawazito.

–         Watu wanaoishi katika nchi ambazo kuna iodini kidogo sana kwenye udongo. Watu ambao hawatumii chumvi ya iodini.

–         Watu wanaokula tu chakula cha mboga.

Uvimbe kwa shingo

Kuvimba kwa shingo ni dalili ya kawaida ya upungufu wa iodini. Hali hii inaitwa goiter na hutokea wakati tezi inakuwa kubwa sana. Tezi hutengeneza homoni za tezi inapopokea ishara kutoka kwa homoni ya kuchochea tezi. Wakati viwango vya damu vinapoongezeka, tezi hutumia iodini kutengeneza homoni za tezi. Walakini, mwili wako unapokuwa na iodini kidogo, hauwezi kutosheleza hivyo tezi hufanya kazi kwa bidii. Hii husababisha seli kukua na kuongezeka na hatimaye kusababisha goiter.

Kuongezeka kwa uzito usiotarajiwa

Kuongezeka kwa uzito usiotarajiwa ni ishara nyingine ya upungufu wa iodini. Hali hii inaweza kutokea ikiwa mwili hauna iodini ya kutosha kutengeneza homoni za tezi. Hii ni kwa sababu homoni za tezi husaidia kudhibiti kasi ya michakato ya kimetaboliki wakati ambapo mwili wako hubadilisha chakula kuwa nishati na joto. Wakati viwango vya homoni za tezi ni vya chini, mwili wako huchoma kalori chache wakati wa kupumzika.

Uchovu na udhaifu

Uchovu na udhaifu pia ni dalili za kawaida za upungufu wa iodini. Watu walio na viwango vya chini vya homoni ya tezi, ambayo hutokea katika hali ya upungufu wa iodini, huhisi uchovu, uvivu na dhaifu. Dalili hizi hutokea kwa sababu homoni za tezi husaidia mwili kutengeneza nishati.

Kupoteza nywele

Homoni za tezi husaidia kudhibiti ukuaji wa mizizi ya nywele. Wakati viwango vyako vya homoni ya tezi viko chini, mizizi ya nywele yako inaweza kuacha kuzaliwa upya. Baada ya muda, hii inaweza kusababisha upotezaji wa nywele.

Ngozi kavu

Ngozi kavu inaweza kuathiri watu wengi wenye upungufu wa iodini. Watu walio na viwango vya chini vya homoni ya tezi wanaweza kupata ngozi kavu na dhaifu. Homoni za tezi, ambazo zina iodini, husaidia seli zako za ngozi kuzaliwa upya. Wakati viwango vya homoni ya tezi ni chini, kuzaliwa upya huku hakutokei mara kwa mara, ikiwezekana kusababisha ngozi kavu na iliyokauka.

Matatizo wakati wa ujauzito

Wanawake wajawazito wako katika hatari kubwa ya upungufu wa iodini. Hii ni kwa sababu wanahitaji kula vya kutosha ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku, pamoja na mahitaji ya mtoto wao anayekua. Ongezeko la mahitaji ya iodini huendelea wakati wote wa kunyonyesha, kwani watoto hupokea iodini kupitia maziwa ya mama.

  • Tags

You can share this post!

Ukweli kuhusu nywele kavu na jinsi ya kumaliza tatizo hili

MAPISHI KIKWETU: Wali wa nyanya

T L