• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
DJ Saint Kevin: Karen Nyamu anaelewa kupenda  

DJ Saint Kevin: Karen Nyamu anaelewa kupenda  

NA MWANGI MUIRURI 

DJ Saint Kevin amemtaja Seneta maalum Karen Nyamu kama mwanamke anayeelewa umuhimu wa kuwa kwenye mahusiano, mlezi bora wa watoto na mama mwenye utu.

Mcheza santuri huyo ndiye baba wa mtoto wa kwanza wa Bi Karen, ambaye kwa sasa anahusishwa na mwimbaji wa nyimbo za Mugithi, Samuel Muchoki maarufu kama Samidoh.

Katika mahojiano na kituo cha radio cha Spice, Kevin alisema kwamba “baada ya kupata binti yetu pamoja na kisha tukaamua kuelekea kila mtu njia yake, huniruhusu nilee mwanangu na kila wikendi humchukua tunaelekea zetu kupiga sherehe”.

DJ Kevin alifichua kwamba alikutana na Nyamu katika hafla moja ndani ya tamasha akipiga shoo.

Alisema kwamba Seneta Nyamu si kazi kukaa naye kama inavyokisiwa na wengi bali “ni mama mwenye roho safi na mlezi mzuri kwa mtoto wangu”.

Akasema: “Karen ni mama mzuri sana…Mimi na yeye hulea binti yetu pamoja…Hakuna sarakasi kati yetu na hakuna mambo yasiyo ya kawaida…Mimi na yeye bado ni marafiki wasio na vituko”.

Alipoulizwa kama bado anafurahia ukoko wa mahusiano yao, DJ Kevin aliangua kicheko akiyakanusha.

“Hapana…Hakuna cha hiyo…Hakuna kabisa hayo mambo…Mimi tu ni kufika wikendi, nachukua mtoto wangu tunaelekea zetu na ni hayo tu,” akasema.

DJ Kevin aliongeza kuwa anaheshimu maisha ya sasa ya Seneta Nyamu na wake, Samidoh ambaye kando na kuwa afisa wa polisi yeye ni msanii.

“Hakuna nwingiliano kamwe…Mimi na Karen tunaishi maisha tofauti kabisa…Mimi ni mimi na maisha yangu na Karen ni yeye na maisha yake. Tunaheshimiana hivyo,” akasema.

Alisema kwamba utaratibu wa kazi yake katika shoo za vilabu ndio ulitia doa kati yake na Karen.

“Haya maisha ya DJ…Kufika nyumbani usiku…Mambo kama hayo na tukaafikiana haikuwa inawiana kamwe…” akasema.

Juni 2023, Karen aliandika kwa mitandao kwamba “DJ Saint ni ex na haina haja niwe namposti”.

Mwaka wa 2021, DJ Kevin alikuwa muwazi kwa upana kuhusu uhusiano wake na Karen na kiini cha kutengana akiwa katika mahojiano na Radio Jambo.

“Uhusiano wetu ulikuwa tu ni ma-fight, ma-fight and for me to decide to leave tulikuwa tumefika a point of no return. Everytime was an argument na sikuwa naona kama ni fair kulea mtoi wetu in that environment. So nika decide nimpatie space yake na mimi niwe na space yangu but it worked out okay. It was getting toxic. Every day was basically a fight,” akasema.

DJ Kevin alimaanisha kwamba uhusiano kati yake na Karen Nyamu, ulisheheni vita visivyoisha.

Alisema shida kubwa ilikuwa Karen kumwagiza asiwe anaingia nyumbani saa za giza totoro “tuseme kwa mfano nisiingie nyumbani saa tisa usiku ilihali naye alikuwa pia anaingia nyumbani saa hizo ananikanya.”

[email protected]

 

 

  • Tags

You can share this post!

Andrew Kibe akaangwa na wafuasi wake mitandaoni

Ndovu wakaidi Taita Taveta ‘wanaonyang’anya’ watu...

T L