• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
DKT FLO: Nini husababisha kinyesi kuchanganyika na damu?

DKT FLO: Nini husababisha kinyesi kuchanganyika na damu?

Mpendwa Daktari,

Ni nini kinachosababisha kinyesi kutoka kikiwa kimechangamana na damu?

Lilian, Nairobi

Mpendwa Lilian,

Melena kwa lugha ya kitaalamu ni hali ambapo kinyesi hutoka kikiwa na rangi nyeusi na husababishwa na damu kuchangamana na kinyesi. Hali hii yaweza ainishwa kulingana na sehemu iliyoathirika kama vile tumbo au utumbo.

Melena ya tumbo au Upper Gastro Intestinal

  • Damu kwenye kinyesi yaweza tokana na vidonda tumboni vinavyosababishwa na mawazo mengi yanayowakumba watu kutokana na hali ya maisha.
  • Oesophagitis au kuvimba kwa mrija wa kupitishia chakula pia kunaweza sababisha kutokwa na damu wakati wa kwenda haja
  • Kula vyakula vyenye viungo vingi
  • Historia ya matumizi ya dawa bila idhini ya daktari hasa ya kupambana na maumivu kama vile aspirini au za kusisimua misuli.
  • Historia ya unywaji pombe
  • Uvutaji wa sigara au utafunaji wa tumbaku
  • Uvimbe katika sehemu ya tumbo
  • Maradhi ya kutokwa na damu kila mara
  • Kumeza damu kwa mfano mtu anapotokwa na damu puani
  • Minyoo tumboni

Ishara za Melena

  • Mgonjwa atalalamikia kubadilika kwa rangi ya kinyesi hadi rangi nyeusi
  • Anemia. Maradhi yanayotokana na upungufu wa virutubisho vya chuma mwilini
  • Udhaifu
  • Kushindwa kupumua
  • Maumivu katika sehemu ya tumbo kutokana na vidonda katika sehemu hii

Ili kuzuia au upambana na hali hii

Kudhibiti hali;

  1. Kula kwa wingi mboga za kijani na hasa zenye kiwango cha juu cha unyuzi
  2. Tumia unga ambao haujakobolewa
  3. Epuka vyakula moto, vilivyokaangwa kwa mafuta mengi au vyenye viungo vingi.
  4. Kunywa glasi moja ya maji kila asubuhi
  5. Kuwa na mazoea ya kwenda choo kila unapohisi haja
  6. Punguza unywaji chai na kahawa
  7. Epuka na unywaji wa pombe na uvutaji sigara
  8. Punguza mawazo mengi
  • Tags

You can share this post!

DKT FLO: Homa ya mapafu inavyosambaa mwilini, dalili na...

‘Nipe nikupe’ ya Ruto na Raila yaendelea

T L