• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Edna Talava alenga makuu katika uigizaji

Edna Talava alenga makuu katika uigizaji

NA JOHN KIMWERE

WAHENGA walilonga kuwa penye nia pana njia.

Na ndivyo ilivyo tangu zama zile hadi sasa. Methali hii inaonekana kuwa na mashiko kwa asilimia fulani miongoni mwa wanajamii.

Vijana wengi, wavulana kwa wasichana, wanaozidi kujitosa kuchangamkia shughuli mbali mbali kwenye jitihada za kujichunia riziki kujikimu kimaisha.

Edna Muthoki Talava ni mmojawapo wa waigizaji wanaoibukia wanaopania kutinga hadhi ya kimataifa miaka ijayo.

Kando na uigizaji mwanadada huyu anafanya biashara ya kuuza mapambo eneo la Murang’a.

”Nilianza kujituma kwenye masuala ya uigizaji nikisoma shule ya upili lakini kuzamia kwa kiasi cha haja nilianza mwaka 2014,” anasema na kuongeza kuwa ingawa hajapata mashiko kwake uigizaji ni ajira kama nyingine.

Anadokeza kuwa nyakati hizi wengi hapa nchini Kenya wameanza kukumbatia uigizaji kinyume na ilivyokuwa miaka iliyopita.

Mwigizaji chipukizi Edna Muthoki Talava anayelenga makuu katika tasnia ya uigizaji miaka ijayo. PICHA | JOHN KIMWERE

Binti huyu amefanya kazi na kampuni nyingi ikiwamo Artspace Production kati ya zingine. Anajivunia kushiriki filamu za Pepeta, Igiza na X Election kati ya nyingine.

Mwanadada huyu tangu utotoni alipania kuwa mshauri wa masuala ya utalii.

Ana ndoto ya kuanzisha brandi yake huku akilenga kuzalisha filamu kusudi kuelimisha jamii katika masula ya maisha kwa kuzingatia filamu sampuli hiyo huwa zinavutia wengi.

Binti huyu mwenye umri wa miaka 26 anasema amepania kupambana mwanzo mwisho akilenga kufikia hadhi ya mwigizaji mahiri Tiffany Hadish mzawa wa Marekani aliyeshiriki filamu kama Like a Boss, Night School, Girls Strip na Nobodys Fool kati ya nyingine.

Tiffany anajivunia kutwaa tuzo kadhaa ikiwamo Grammy Awards kitengo cha Best Comedy Album. Pia tuzo ya Primetime Emmy Awards kitengo cha Outstandings Guest Actress in a Comedy Series.

Hapa nchini angependa kufanya kazi na waigizaji kama Sarah Hassan aliyeshiriki Crime and Justice, Plan B, Zora pia Jackie Matubia aliyeshiriki Zora na Tahidi High.

Afrika anatamani sana kufanya kazi na waigizaji ambao hushiriki filamu za Nollywood na ambao ni Jackie Appiah na Mercy Johnson.

Anashikilia Nollywood inazidi kufanya vizuri katika uigizaji maana wasanii hushikana mikono bila kubaguana.

Kama ilivyo kawaida ya waigizaji wengi anasema amekubana na changamoto kibao ikiwamo kusafiri maeneo ya mbali kushiriki uigizaji wa vitabu vya kutahiniwa katika shule za upili – setbooks – na kupata malipo duni.

Anashauri wenzie wanaokuja kuwa wasiwe wepesi kutamani mafanikio bali wafahamu wakati wa Mungu ndio mzuri.

”Wengi tu tunapenda kufikia mafanikio lakini kabla ya muda wake Mungu Muumba kutimia hata tukijituma kwa kiwango gani kamwe hatuwezi kutimiza malengo yetu,” anasema.

Anadokeza kuwa wengi wao wana vipaji lakini hushindwa kujitambua na kujihusisha na masuala ambayo baadaye huwaaribia taaluma zao.

Anaelezea wenzie wanaoibukia wawe wabunifu endapo wanapania kupenya katika sekta ya burudani.

Aidha anawahimiza kuwa wafahamu hakuna mafanikio huja rahisi lazima wamakinike kama sivyo ni rahisi kuangukia meno ya maprodusa ambao hupenda kushusha hadhi ya wasanii wa kike.

  • Tags

You can share this post!

Raila akataa kushiriki mdahalo wa urais

Ukraine: Mkataba wasifiwa na US, EU

T L