• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 2:00 PM
Faida za ‘beetroot’

Faida za ‘beetroot’

Na MARGARET MAINA

[email protected]

‘BEETROOT’ au tini ni chakula kinachoweza kubadilika ambacho kinaweza kuliwa kikiwa kibichi, kwenye saladi na sharubati au kupikwa na kuongezwa kwa lishe kuanzia kifungua kinywa hadi chakula cha jioni.

Mbali na protini za nyuzi na mboga, beetoot pia ina magnesiamu, potasiamu, shaba, chuma, vitamini C na vitamini za kikundi B.

Sharubati ya beetroot ni kinywaji maarufu kote duniani.

Beetroot ina vitamini na madini mengi ambayo husaidia kukabiliana na magonjwa ya viungo na mifumo mbalimbali.

Beetroot inaongeza kiwango cha juu cha hemoglobin katika damu kutokana na chembechembe za chuma yaani iron.

Inapambana vizuri na edema na kuvimbiwa kutokana na athari za majimaji yaliyopitiliza katika nyama za mwili. Inapambana kwa kusaidia mkojo kutoka kwa wingi hali inayojulikana kama diuretic na pia husaidia kulainisha choo cha binadamu ikitumika kama laxative.

Inaboresha rangi na ngozi kwa ujumla.

Beetroot pia husaidia kusafisha ini, figo na mishipa ya damu.

Inakabiliana na lehemu “mbaya”.

Inaboresha hali ya mwili kwa ujumla.

Inaongeza kiasi cha oksijeni inayoenda kwa moyo na misuli kupitia upanuzi wa mishipa ya damu.

Rangi nyekundu, zambarau, au rangi ya beetroot ni kiashiria bora cha yaliyomo kwenye antioxidant.

Kwa sababu ya antioxidants zake, beetroot pia ni muhimu sana katika kulinda afya ya macho.

Betaine na choline vimeonyeshwa kudhibiti kwa nguvu mapigo ya moyo na mishipa hivyo husaidia kupunguza viwango vya lehemu na shinikizo la damu.

Kwa sababu ya kiwango cha juu cha madini ya chuma kwenye beetroot, ulaji mboga au juisi yake husaidia kujaza kirutubisho hiki.

Ikiwa tuna madini ya chuma ya kutosha katika damu yetu, hewa tunayopumua inaweza kusafirishwa vyema kwa mwili wote.

You can share this post!

Zuma atakiwa ajiamulie kifungo anachotaka apewe

Faida za kula malenge