• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
Faida za kula malenge

Faida za kula malenge

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MALENGE yako katika kundi la maboga yaliyo na vitamini.

Carotene iliyoko kwenye malenge, inasaidia katika kudumisha afya ya ngozi, kuboresha mfumo wa neva, njia ya kupumua na njia ya utumbo. Vitamini A ni muhimu sana wakati wa ujauzito.

Mbegu za malenge zina protini, vitamini na asidi ya mafuta ya Omega-3. Malenge pia yana kiasi kikubwa cha vitamini B, pamoja na kalsiamu, potasiamu na fosforasi.

Malenge husaidia katika mipango ya kupunguza uzani. Mbegu za malenge zina nyuzi bora na asidi ya mafuta ambayo husaidia mwili katika mchakato wa kupoteza au kupunguza uzani.

Vipande vya malenge. Picha/ Margaret Maina

Faida za malenge kwa ini

Wale ambao wanakabiliwa na Hepatitis A ya virusi, wanaweza kujumuisha juisi ya malenge ya asili katika chakula chao cha kawaida. Ni bora kujipikia nyumbani kwako mwenyewe.

Malenge yanatumika katika diuretic ili kusaidia mkojo kutoka kwa wingi hasa kwa watu wenye matatizo ya figo. Malenge mabichi yanapendekezwa kwa watu walio na matatizo ya figo na pia kwa kuzuia kifua kikuu.

Malenge ni antioxidant ambayo ina umuhimu mkubwa hasa katika kuzuia michakato yoyote ya wadudu kwenye kiwango cha seli.

Kwa wale ambao ni wanene sana au wanajitahidi na wanahangaika, malenge husaidia kupunguza uzani uliopitiliza.

Kwa watu ambao hucheza michezo – mazoezi ya kuchoma mafuta yanayosababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu ni maarufu sana sasa – hivyo vipande kadhaa vya malenge vitasaidia kurekebisha shinikizo la damu.

Malenge hayana vitamini A nyingi lakini ulaji wake husaidia kuimarisha nuru ya macho japo kidogo.

Malenge yana vitamini C nyingi, ambayo inasaidia mfumo wa kinga.

Malenge ni mazuri pai katika kuimarisha mfumo wa umeng’enyaji wa chakula tumboni.

Afya ya binadamu ni utaratibu mgumu ambao unahitaji kufuatiliwa kwa uangalifu, na malenge ni msaidizi bora katika suala hili. Ikiwa mboga hii iko kwenye lishe yako kila wakati, afya yako itaimarika, na mifumo yako na viungo vitafanya kazi vizuri.

Kwa wale ambao wanahusika katika michezo ya kujitutumua sana, mbegu za malenge zitasaidia “kujenga” na sio kupoteza misuli.

You can share this post!

Faida za ‘beetroot’

Wakazi wa Gatundu Kaskazini wataka walipwe fidia