• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
HUKU USWAHILINI: Corona imeanika mikataba feki ya mapenzi huku kwetu

HUKU USWAHILINI: Corona imeanika mikataba feki ya mapenzi huku kwetu

NA SIZARINA HAMISI

HUKU Uswahilini kipindi hiki ambacho kuna sintofahamu nyingi za kiuchumi, kutiliana shaka na hata kutengana yamekuwa ni mambo ya kila wakati.

Mtaani kwetu tumeshuhudia wakikurupushana na kutengana sababu ya changamoto za kiuchumi ambazo huhamia katika uhusiano.

Katika pitapita zangu nikadodosa kwa akina dada ambao wameachana na wenzao, nao suala lao kubwa lilikuwa ni kwamba hao wapenzi wao hawaonyeshi kujali tena.

Nikaambiwa wao waliwapenda waume zao kwa dhati na hata walikuwa tayari kuishi katika changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na kukosa kazi sababu ya madhara ya janga la corona.

Akaniambia shambenga wa mtaani; “dada unapopenda kwa dhati, tegemeo kubwa ni kwamba, mwenzako pia akupende kwa vitendo na siyo maneno matupu. Wengine tuko tayari kuishi nao bila pesa, lakini wenyewe hawaonyeshi kutujali hata chembe…”

Na hivi leo nataka nikubaliane na hoja ya akina dada hawa, kwani baadhi ya walio katika uhusiano, wanalalamika kuwa, wenzao hawawapendi kwa kiwango wanachotamani kupendwa.

Ni vyema ikatambulika kuwa, japokuwa mapenzi huchukuliwa kama jambo la kawaida, kumpenda mtu mwingine kwa dhati, huhitaji mbinu na mikakati.

Ukweli ni kwamba, hakuna mwanamke au mwanamume anayeweza kumpenda mtu kisirani, mlalamishi na asiyependa maelewano.

Ni nani atampenda mwanamume mvivu, asiyejituma na mwenye kupenda zaidi starehe na watu wengine, huku akimsahau mwenzake?

Kuna mbinu za kumfanya mwandani wako azidi kukupenda na kukujali.

Baadhi ya akina dada hudhani urembo pekee unatosha kuwafanya wapenzi wao wazidi kuwapenda na kuwajali.

Lakini uzuri wa mwanamke siyo sura pekee. Mwenendo na vitendo, ndivyo huangaliwa kwa kiasi kikubwa.Hakuna mwanamume ambaye atafurahia kuwa na mwanamke kiburi na asiyeonesha kumjali wala kumthamini.

Ni kiu ya kila mwanaume kuwa mfalme kwa mke wake. Yaani awe na kauli juu yake, awe na uwezo wa kutoa maelekezo na yakatekelezwa.

Hata kama familia mnapitia kipindi kigumu cha uchumi, si jukumu lako mwanamume kila muda kukaa na kulalamikia hali hiyo.

Pambana na hali yako.

Huku uswahilini watu wanahitaji kupendwa pia, sio kwa maneno bali vitendo.

You can share this post!

TAHARIRI: Serikali inafanya mzaha na mtaala wa CBC

FATAKI: Vipodozi haviongezi wala kupunguza werevu wako,...

T L