• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Maandamano: Maina Kairu, mwenyekiti wa Azimio Nakuru amsaliti Raila Odinga 

Maandamano: Maina Kairu, mwenyekiti wa Azimio Nakuru amsaliti Raila Odinga 

NA SAMMY WAWERU

MWENYEKITI wa Azimio la Umoja tawi la Nakuru Mashariki, Maina Kairu amejitenga na maandamano ya muungano huo, akihoji msimamo wake haumruhusu kuyashiriki. 

Bw Kairu alisema Jumapili, Julai 23, 2023 kwamba sera zake zinaegemea maendeleo ila si siasa za ukandamizaji uchumi. 

Licha ya kujiondoa na maandamano yaliyoitishwa na kinara wa Azimio, Bw Raila Odinga, afisa huyo alisisitiza kuwa maamuzi yake hayaashirii kusaliti yeyote. 

Badala yake, Kairu alisema “Sijasaliti yeyote na ikiwa kuna niliyesaliti, ni mimi mwenyewe nimejisaliti; Nimeenda kinyume na niliyoamini kwa sababu naona hayafai”. 

Mwenyekiti huyo wa Azimio Nakuru Mashariki, alisema chini ya muda mfupi ambao serikali ya Kenya Kwanza inayoongozwa na Rais William Ruto imekuwa madarakani, imemthibitishia kuwa na uwezo kuboresha maisha ya Wakenya. 

“Mimi ninaona bei ya chakula, kama vile viazi imeanza kushuka. Hilo limetokana na mpango wa fatalaiza ya bei nafuu, na hivi karibuni hata bei ya unga itashuka,” alielezea. 

Kairu alisema tayari anaendelea kuzungumza na wafuasi wake, kuepuka kushiriki maandamano. 

Upinzani umeitisha maandamano ya siku tatu kila wiki, kushinikiza serikali kushusha gharama ya maisha. 

Maandamano hayo yaliyoharamishwa na serikali, yamesababisha maafa ya watu kadhaa kutokana na risasi, baadhi wakiuguza majereha mabaya na mamia kukamatwa. 

  • Tags

You can share this post!

Machimbo hatari Soy yaliyoangamiza watoto wawili

Panzi wazua hofu wakiharibu mimea

T L