• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 1:56 PM
MALENGA WA WIKI: Tungo za Muyaka zilikuwa chachu ya uandishi wa Boukheit Amana

MALENGA WA WIKI: Tungo za Muyaka zilikuwa chachu ya uandishi wa Boukheit Amana

Na HASSAN MUCHAI

MAISHA yake ya utotoni, Boukheit alikua kama watoto wengi wa pwani.

Michezo yao huwa aghalabu inahusiana na bahari. Kutengeza vidau vidogo vinavyoshabihi madau wanayotumia wazazi wao kwa usafiri na uvuvi.

Alipenda mchezo wa mpira wa miguu ijapokua haikuwa kiwango cha magwiji wa mchezo huo.

Alipokuwa Shule ya Msingi ya Serani aliwahi kuiwakilisha shule hiyo kwenye mchezo wa kuruka juu (high jump) na kuishindia kikombe kwenye uwanja wa manispaa (stadium).

Wakati wa likizo alikuwa akiandamana na babake kwenda baharini kwenye shughuli za uvuvi.

Siku za awali kwenda baharini alikuwa na kicho anapoona mawimbi yakipanda na kushuka. Siku nyingine Boukheit alikuwa akijumuika na vijana wenziwe kuogelea tu.

Aghalabu waliogelea kutoka soko la samaki liitwalo Forodhani lililoko sehemu za mji wa kale maarufu Old town. Kwa akili za kitoto, bila kuogopa hatari zilizoko baharini, Boukheit na wenzake walikuwa wakishindana kuogelea hadi ng’ambo ya pili ijulikanayo kama Mkomani.

Ushairi

Ari ya uandishi ilijitokeza alipokuwa kidato cha tatu wakati wanafunzi wa Coast Girls Secondary School Mombasa walimsihi awatungie tamthilia watakayoitumia kwenye mashindano ya shule ya mikoa.

Tamthilia hiyo kwa jina Zabibu Chungu baadaye ilichapishwa na shirika la Oxford. Utunzi wa mashairi alianza wakati huo akiwa kidato cha tatu. Vitabu vilivyomtia moyo wa utungaji ni kama vile vya Kaluta Amri Abedi, Shaaban Robert, Mathias Mnyampala, Malenga wa Mvita na vinginevyo.

Maandishi ya Muyaka bin Haji yalikuwa na lugha pevu ambayo ilikuwa si rahisi kulingana na umri aliokuwa nao kuelewa.

Kutokana na athari za mahiri hao aliwahi kuandika nakutuma magazetini. Kama si jicho pevu la mmoja wa walimu wake, Muhammad Bakari ambaye sasa ni profesa pengine tusingejua kipawa alichokuwa nacho Boukheit.

Profesa Muhammad Bakari ndiye aliyepeleka mswada huo Oxford. Wakati huo Boukheit alikuwa akitumia lakabu ya Mti mle kujitambulisha kishairi. Wale waliowahi kuupitia uandishi huo, Muhammad Kamal Khan na Hassan Msami ndio waliafikiana kumpa lakabu ya Malenga wa Vumba.

Mwandishi wetu ameandika baadhi ya mashairi yake kwa lugha hii ya Kivumba. Vumba ama pia Vanga, ni mji ulioko kusini mwa Kenya, ambako ndiko asili ya mamake Boukheit. Wenyeji wa huko wanaitwa Wavumba, wengi wao ni masharifu.

Vanga imepakana na Shirazi na Wasini. Upande wa Tanzania ni jirani na mji wa Moa ambao lugha yao ni moja. Mfano wa Wamaasai, Wajaluo, Wakuria na wengineo ambao wanaishi mipakani ya nchi mbili hizi.

Kitabu chake cha Malenga wa Vumba kimewahi kunukuliwa na waandishi wengi wa ushairi wa Kiswahili. Sababu moja ya umaarufu wa diwani hii ni kua mwandishi alitumia aina na bahari tofauti za mashairi. Toleo Jipya la Malenga wa Vumba ambalo halikupoteza uasilia wake lina marekebishko na nyongeza muafaka. Moja katika marekebisho hayo yako kwenye shairi lililo kwenye utangulizi;Rara lirarile rara

You can share this post!

Korti yafungua miradi ya mabilioni ya pesa Pwani

Hapa udikteta tu