• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
MALEZI KIDIJITALI: Teknolojia inajenga na kuumbua familia vilevile

MALEZI KIDIJITALI: Teknolojia inajenga na kuumbua familia vilevile

TEKNOLOJIA inatawala kila sehemu ya maisha katika karne hii na wazazi wasiokubali au kujiandaa wanaweza kuathiri malezi ya watoto wao na familia kwa jumula.

Maisha ya familia yakiwemo malezi yanaendelea kubadilika teknolojia inavyozidi kustawi.

Wataalamu wanasema kuwa kila shughuli ya maisha ya familia imebadilishwa na teknolojia inayojiri na faida na hatari zake pia.

“Kuendelea kuibuka kwa teknolojia kunamaanisha kuwa familia ambayo ni msingi wa jamii imebadilishwa na vifaabebe, kompyuta na teknolojia zingine za dijitali. Familia inaathiri pakubwa ukuaji wa mtu binafsi na mtazamo wake kuhusu jamii na sasa inashawishi jinsi mtu anatangamana na teknolojia,” unasema utafiti wa Chuo Kikuu cha Edinburgh kuhusu athari za teknolojia kwa familia, inavyoshawishi malezi na jamii kwa jumula.

Utafiti huo unasema kwamba uhusiano kati ya mzazi na mtoto unaamua mahusiano mengine yatakavyokuwa katika maisha yake na teknolojia katika familia inaunda mtazamo wa mtu kuhusu maisha ya kijamii katika ulimwengu wa dijitali.

Katika familia, teknolojia ya dijitali inaweza kuwa chanzo cha vurugu au kuunganisha.

Katika kitabu chao kuhusu malezi dijitali, Networked, waandishi wanasema kwamba teknolojia imefanya familia kutokuwa na wakati mwingi wa kuonana uso kwa uso lakini ziko na wakati mwingi wa kuwasiliana kwa sababu ya mabadiliko ya teknolojia.

Wanasema kuwa hii hasa inasababishwa na wanawake wengi kujiunga na ajira na kupunguza au kukosa muda wa kuwa na familia zao ikiwemo kujali maslahi ya watoto.

“Wanawake wamepunguza muda wanaotumia kwa majukumu ya nyumbani, ingawa wanatekeleza maradufu kuliko wanaume,” wanaeleza waandishi wa kitabu hicho.

Wataalamu wanasema kwa sababu ya shinikizo za kazi, wazazi wengi huwa wanashinda mtandaoni na kukosa muda wa kutosha na watoto wao. Hii inaathiri uthabiti wa familia na jamii kwa jumla.

“Matokeo ni jamii tunayoshuhudia kwa sasa isiyojua inakotoka na inakoelekea. Isiyojali kwa kuwa familia zimeathiriwa na teknolojia inayopaswa kustawisha jamii,” wasema utafiti wa Chuo Kikuu cha Edinburgh.

You can share this post!

Nottingham Forest wazamisha chombo cha Liverpool katika EPL

HUKU USWAHILINI: Bwana, huwa tunajichosha huku sherehe hadi...

T L