• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 11:50 AM
MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa uduvi almaarufu ‘shrimps’

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa uduvi almaarufu ‘shrimps’

NA MARGARET MAINA

[email protected]

JE, unatafuta chakula cha ama chamcha au chajio cha haraka sana, lakini kitamu?

Uduvi wa sosi unakuwa na ladha tamu na ukiongeza marinadi ya asali, mchuzi wa soya, na vitunguu, basi kila atakayekila chakula hicho atapenda.

Kwa ladha ya ziada kidogo, tunaongeza tangawizi safi iliyokatwa, lakini hiyo ni hiari.

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • kikombe ¼ cha asali
  • kikombe ¼ cha sosi ya soya (tumia yenye sodiamu iliyopunguzwa)
  • punje 3 za vitunguu saumu na hakikisha punje zimesagwasagwa
  • kwa hiari: kijiko 1 cha tangawizi iliyokatwa
  • kilo 1 ya uduvi wa kati ambao hawajapikwa na ambao wamevuliwa na kutengenezwa
  • vijiko 2 vya mafuta ya alizeti
  • hiari kwa ajili ya kupamba, vitunguu vya kijani

Chakula kikiwa kimeshaiva tayari kuliwa. Uduvi ni samaki wadogo wa jamii ya kamba. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Changanya asali, sosi ya soya, kitunguu saumu na tangawizi (ikiwa unatumia) pamoja kwenye bakuli la wastani.

Utatumia nusu kwa marinadi katika hatua ya pili na nusu kupika uduvi katika hatua ya tatu.

Weka uduvi kwenye chombo kikubwa kinachozibika au mfuko uliofungwa juu.

Mimina nusu ya mchanganyiko wa marinadi /mchuzi juu, tikisa yote au koroga, kisha ruhusu udavi kugandamana kwenye jokofu kwa muda wa kati ya saa 8 hadi 12.

Funika na uweke kwenye jokofu marinadi iliyobaki kwa hatua ya tatu.

Pasha mafuta ya mzeituni kwenye sufuria juu ya moto wa kati.

Weka uduvi kwenye sufuria, ongezea marinadi iliyobaki kwa juu. Pika uduvi upande mmoja hadi kuwa na rangi ya hudhurungi (muda wa kama dakika mbili hivi) kisha pindua uduvi juu.

Mimina katika marinadi iliyobaki / mchuzi na upike vyote hadi viive na viwe tayari (itakuchukua kama dakika tano zaidi).

Pakua uduvi na mchuzi wa marinadi iliyopikwa. Unaweza kupamba chakula chenyewe kwa vitunguu vya kijani.

Mchuzi huu wa uduvi ni bora kwenye wali na mboga mchanganyiko.

  • Tags

You can share this post!

Masharti mapya ya maridhiano yazuka

Ole wenu mliomtamani, Akothee aoleka na mchumba wake mzungu

T L