• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 10:50 AM
MAPISHI KIKWETU: Kuandaa viazi na samaki mbichi

MAPISHI KIKWETU: Kuandaa viazi na samaki mbichi

NA PAULINE ONGAJI

1. Chemsha viazi kwa muda wa dakika 8

2. Ongeza spinachi kisha uache mchanganyiko uendelee kutokota kwa muda zaidi hadi viazi viive na kunyooka. Kamua maji yaliyosalia

3. Huku kiwango cha moto kikiwa ni cha kati, tia mafuta kwenye karai kubwa.

4. Tia viazi, spinachi na maharagwe, kitunguu saumu kijiko kimoja cha chai, pilipili tamu.

5. Kaanga kwa muda huku ukipindua viazi ukitumia uma hadi vinyooke zaidi, vionekane kuyeyuka kwa umbali na kubadili rangi na kuwa hudhurungi hafifu. Hakikisha kuwa viungo vyote hasa chumvi, vimekolea.

6. Nyunyiza pilipili tamu iliyosagwa juu ya chakula, funika karai kisha weka katika moto wa kiwango cha kati kwa dakika zisizopungua 3 na zisizozidi 10.

7. Kwenye sufuria tofauti, tia mafuta ya mboga ya kukaanga, vijiko vya meza 3. Ongeza vitunguu, endelea kukaanga kwa muda hadi vibadili na kuwa rangi ya hudhurungi hafifu.

8. Tia nyanya na kitunguu saumu, koroga kwa muda kisha ufunike kwa dakika 3 au hadi mchanganyiko uwe mwepesi na kuwa rangi nyekundu.

9. Ongeza maji moto vikombe 2, kisha ufunike, hadi mchuzi utokote. Kwa utaratibu, tia vipande vya samaki, huku ukihakikisha vimefunikwa na mchuzi.

10. Funika kwa dakika 15 au hadi vipande viive. Koleza kwa chumvi na pilipili, kisha ufunike kwa dakika 5 zaidi.

11. Kwenye sinia andaa viazi vilivyokaanga pamoja na kitoweo cha samaki.

You can share this post!

Sipangwingwi: Washirika wa Ruto wakaidi NCIC

Man-City na Liverpool bado unyo kwa unyo katika EPL baada...

T L