• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
MAPISHI KIKWETU: Pilau yenye uyoga na njegere

MAPISHI KIKWETU: Pilau yenye uyoga na njegere

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 50

Walaji: 3

Vinavyohitajika

  • vikombe 1 ½ vya mchele wa pishori
  • vijiko 2 vya pilau masala
  • punje 5 za kitunguu saumu; hakikisha unasagasaga
  • kitunguu maji chekundu kilichokatwa vipande vipande
  • jani 1 la bay
  • kijiko 1 cha jira
  • chumvi kwa ladha
  • kijiko 1 cha nyanya ya kopo
  • kikombe cha njegere zilizochemshwa
  • kikombe 1 uyoga

Maelekezo

Katika sufuria, weka kitunguu chekundu, kitunguu saumu na chumvi kidogo. Pika hivi hadi viwe na rangi ya hudhurungi ya dhahabu. Jihadhari visiungue bali viwe na rangi ya kahawia. Hii ni hatua muhimu ya kupata rangi hiyo nzuri ya kahawia ya pilau.

Pilau masala ni mchanganyiko wa viungo unaojumuisha viungo vifuatavyo: pilipili nyeusi, jira, karafuu, mdalasini na iliki.

Unaweza kujitengenezea nyumbani na kubadilisha uwiano wa viungo vilivyotajwa ili kukidhi ladha yako.

Vitunguu vikishakuwa na rangi ya kahawia, weka nyanya ya kopo, pilau masala yako iliyosagwa na acha hii iive hadi ichanganyike kabisa. Watu wengine hawatumii nyanya. Kisha ongeza uyoga.

Uyoga. PICHA | MARGARET MAINA

Ikiwa ungekuwa ukipika pilau ya nyama ya ng’ombe au kuku, ungeongeza pia katika hatua hii. Tofauti tu ni kuwa, utapika kwa muda mrefu zaidi kuliko uyoga.

Ongeza uyoga, changanya na baada ya dakika mbili, ongeza maji na wali wako.

Pika hadi maji yapungue kiasi cha robo tatu kisha ongeza njegere. Zinaongezwa kuelekea mwisho kwa sababu tayari zimepikwa.

Changanya njegere kwenye wali taratibu kwa uma, kisha funika na kifuniko na kuruhusu pilau kumaliza kupika.

Kisha baada ya kuiva, pakua na kachumbari na ufurahie.

Pilau yenye uyoga na njegere. PICHA | MARGARET MAINA

 

  • Tags

You can share this post!

Njia za asili za kupunguza viwango vyako vya lehemu

CECIL ODONGO: Itakuwa mwisho wa Ford-Kenya na ANC...

T L