• Nairobi
  • Last Updated May 15th, 2024 8:55 PM
MAPISHI KIKWETU: Supu ya karoti na majani ya giligilani

MAPISHI KIKWETU: Supu ya karoti na majani ya giligilani

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 15

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • mafuta ya kupikia
  • kitunguu maji kilichokatwakatwa
  • karoti 4
  • punje 5 za kitunguu saumu
  • mchuzi wa mboga
  • majani ya giligilani
  • vijiko 3 vya giligilani ya poda
  • maji ya limau vijiko 2
  • kungumanga ya poda kijiko 1
  • chumvi
  • pilipili nyeusi
Supu ya karoti. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Osha na ukatakate karoti kwa vipande.

Pasha mafuta kwenye sufuria kubwa mekoni na kaanga vitunguu maji, karoti na vipande vya kitunguu saumu ulivyokatakata kwa dakika nne.

Mara baada ya kuwa laini, ongeza giligilani ya poda, chumvi na pilipili nyeusi na ukoroge.

Mimina mchuzi wa mboga kwenye sufuria. Funika sufuria na uiruhusu kuchemsha hadi karoti ziwe laini – kama dakika 15.

Koroga kisha ongeza majani ya giligilani, ondoa kutoka kwa moto na uongeze maji ya limau, kungumanga na viungo vinginevyo unavyopenda.

Unaweza kutumia blenda kuchanganya supu yako.

Supu itakuwa imepoa wakati inachanganywa, kwa hivyo ikiwa unapanga kula mara moja, pasha tena supu kwa upole, bila kuichemsha, na uitumie.

Ikiwa unaihifadhi kwa ajili ya baadaye, iruhusu ipoe na kuiweka kwenye chombo kisichopitisha hewa kwenye jokofu.

  • Tags

You can share this post!

WANTO WARUI: Walimu wakuu watashindwa kugharimia bei ya juu...

LISHE: Matunda ya pitahaya/ matunda ya joka

T L