• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Miguna Miguna akosa kwenye orodha ya uteuzi wa DPP

Miguna Miguna akosa kwenye orodha ya uteuzi wa DPP

NA SAMMY WAWERU

MAJINA ya wakili na mwanaharakati Miguna Miguna yamekosa kwenye orodha ya uteuzi kusaka Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma (DPP).

Nafasi hiyo ilisalia wazi baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, Noordin Haji kuteuliwa na Rais William Ruto kuongoza kitengo cha ujasusi nchini, NIS).

Bw Miguna Miguna alikuwa miongoni mwa waliotuma barua ya maombi kumrithi Bw Haji.

Majina ya wakili huyo tajika hasa kukashifu kupitia mitandao ya kijamii wanaomkosea na pia uongozi mbaya, hayakuonekana kwenye orodha ya watakaopigwa msasa.

Wawaniaji 15 waliorodheshwa.

Thomas Letangule, wakili na aliyewahi kuhudumu kama Kamishna katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Taib Ali Taib, wakili Danstan Omari, Francis Andayi Weche, Tabitha Wanyama, James Wahome, ni kati ya waliorodheshwa kuhojiwa na kamati kusaka DPP.

Saba wa kwanza, watahojiwa mnamo Jumanne, Agosti 1, 2023, nalo kundi la pili lenye wawaniaji 8 Jumatano, Agosti 2.

  • Tags

You can share this post!

Wazee na wachungaji wabishania tohara ya vijana wa Agikuyu

Familia yalilia haki baada ya mwana wao kuuawa kwa risasi...

T L